• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 5:46 PM
Ugawaji usiofaa wa fedha kwa shule wasukuma walimu kufanya michango

Ugawaji usiofaa wa fedha kwa shule wasukuma walimu kufanya michango

Na OUMA WANZALA

MBINU mbaya za kugawa pesa za ujenzi wa miundomsingi katika shule za upili nchini imelazimu shule nyingi kuwa zikiandaa hafla za kuchangisha pesa ili kujenga madarasa, mabweni na vyoo.

Hii ni licha ya wizara ya Elimu kutenga Sh439 milioni kwa shule hizo.

Maafisa wakuu serikalini, akiwemo Naibu Rais William Ruto wamekuwa wakizunguka kote nchini kushiriki hafla za uchangishaji pesa kwa ujenzi wa shule, ili kufanikisha mradi wa wanafunzi wote wanaomaliza shule za msingi kuingia shule za upili.

Lakini shule nyingi bado zinaripotiwa kuwa zimekuwa zikipokea pesa chache kutoka kwa serikali ikilinganishwa na shule za kitaifa, hali ambayo imelazimu walimu wakuu kugeukia wanasiasa kwa msaada.

Kwa mfano, wiki iliyopia Naibu Rais na kiongozi wa chama cha ANC walikuwa katika shule tofauti kusaidia katika uchangishaji wa pesa za maendeleo. Kwa upande mwingine, Gavana wa Busia Sospeter Ojaamong na mbunge wa Matayos Geoffrey Odanga walikuwa katika shule ya Our Lady of Mercy Girls, kuchangisha pesa za ujenzi wa bweni.

Hivi ndivyo hali imekuwa kwa shule nyingi kila zinapotaka kutekeleza mradi, kutokana na hali ya kukosa pesa.

“Tunaomba hizi pesa ziwe zikitolewa kwa usawa. Zinafaa kupewa shule lakini wanaojuana ndio wanapata. Hii si njia nzuri ya kugawa rasilimali za umma,” Gavana Ojaamong akamuomba waziri wa Elimu George Magoha.

Rais Uhuru Kenyatta wiki iliyopita alisisitiza kuwa serikali yake inatilia maanani ujenzi wa miundomsingi mashuleni kuanzia mwaka wa Fedha unaoanza Julai, ambapo aliwaomba wabunge kuunga bajeti ya kazi hiyo mkono.

You can share this post!

Shujaa yaning’inia pabaya Raga ya Dunia

Red Cross yatetewa na wabunge

adminleo