• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Lawrence Cherono aibuka mshindi Boston Marathon, apokea Sh15m

Lawrence Cherono aibuka mshindi Boston Marathon, apokea Sh15m

Na GEOFFREY ANENE

LAWRENCE Cherono ametwaa taji la Boston Marathon nchini Marekaeni, huku Mkenya mwenzake Edna Kiplagat akiridhika katika nafasi ya pili ya nchini Marekani, Jumatatu.

Cherono alimpiku Lelisa Desisa kwenye laini akinyakua taji kwa saa 2:07:57, sekunde 0.02 mbele ya Muethiopia huyo.

Kenya ilifagia nafasi tatu zilizofuata kupitia kwa Kenneth Kipkemoi (2:08:07), Felix Kandie (2:08:54) na bingwa wa mwaka 2017 Geoffrey Kirui (2:08:55).

Muamerika Jared Ward (2:09:25) na Wakenya Festus Talam (2:09:25) na Benson Kipruto (2:09:53) walikamilisha wakimbiaji 10 wa kwanza. Bingwa mtetezi Yuki Kawauchi kutoka Japan alimaliza katika nafasi ya 17 karibu dakika nane baada ya Cherono kukata utepe (2:15:29).

Muethiopia Worknesh Degefa alishinda kitengo cha kinadada baada ya kuchukua uongozi kutoka kilomita ya sita hadi utepeni.

Wanariadha wala chajio usiku wa kuamkia Boston Marathon. Picha/ Hisani

Malkia wa Riadha za Dunia mwaka 2011 na 2013 Kiplagat, 39, alikuwa anatafuta kurejesha taji la Boston alilolishinda mwaka 2017. Degefa,29, alitumia saa 2:23:31 kumamilisha umbali huu wa kilomita 42.

Kiplagat, ambaye alikamilisha Boston Marathon katika nafasi ya tisa mwaka 2018, alikamilisha kwa saa 2:24:13 akifuatwa kwa karibu na Muamerika Jordan Hasay (2:25:20), Muethiopia Meskerem Assefa (2:25:40) na bingwa mtetezi Desiree Linden kutoka Marekani (2:27:00).

Wakenya Caroline Rotich (2:28:27) na Mary Ngugi (2:28:33) walifuatana katika nafasi za sita na saba mtawalia. Muethiopia Biruktayit Eshetu (2:29:10), Muamerika Lindsay Flanagan (2:30:07) na Mkenya Betsy Saina (2:30:32) walikamilisha nafasi 10 za kwanza.

Makala haya ya 123 yalivutia watimkaji 30, 000, huku nafasi 10 za kwanza zikiandamana na tuzo ya Sh15.1 milioni, Sh7.5 milioni, Sh4 milioni, Sh2.5 milioni, Sh1.5 milioni, Sh1.2 milioni, Sh909,000, Sh747,400, Sh575,700 na Sh424,200, mtawalia.

You can share this post!

Ushuru na Wazito washuka NSL

Korti yawaachilia wanakamari 13 wakasajiliwe Huduma Namba

adminleo