• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Zingatieni sheria za barabarani Pasaka hii, madereva waambiwa

Zingatieni sheria za barabarani Pasaka hii, madereva waambiwa

Na CHARLES WASONGA

IDARA ya Polisi imewataka wenye magari kuzingatia sheria za barabara katika msimu wa Pasaka ili kuzuia maafa kupitia ajali za barabarani.

Akiongea na wanahabari katika makao makuu ya idara hiyo jumba la Vigilance, Bw Owino alisema dereva yeyote ambaye atapatikana akivunja sheria za barabarani atapokonywa leseni kando na kuhukumiwa kifungo gerezani.

“Wale ambao watapatikana wakiendesha magari wakiwa walevi, wakiendesha magari mabovu au wenye matatu ambao watapatikana wakihudumu katika ruti ambazo hawajaidhinishwa kutumia pia watapokonywa leseni,” akaongeza Bw Owino ambaye alikuwa ameandamana na Mkurugenzi Mkuu wa Halmashauri ya Usalama Barabarani (NTSA) Francis Meja.

“Ajali nyingi hufanyika nyakati za usiku na husababishwa na magari ya uchukuzi wa abiri ambayo hutumia ruti ambazo hayakaidhinishwa kuhudumu,” akaongez.

Aidha, Bw Owino aliwaonya polisi wa trafiki dhidi ya kuwahangaisha wenye magari ya uchukuzi kwa sababu ya makosa madogo.

“Wakati mwingine utapata mwenye matatu hakihangaishw kwa sababu mikanda michafu. Ikiwa mkanda wa usalama unaweza kutumika, dereva haifai kukamatwa,” akasema.

Kulingana na takwimu kutoka kwa NTSA jumla ya watu 184 walifariki katika ajali za barabarani.

Idadi ya watu wanaofariki katika ajali za barabarani imekuwa ikiongezeka tangu mwaka wa 2016. Jumla ya watu 26 walifariki katika ajali za barabarani mwaka huo, watu 39 wakafa mnamo 2017 na 2018 jumla ya watu 37 waliangamia wakati msimu huo katika ajali za barabara.

Bw Meja alisema ajali nyingi hushuhudiwa katika barabara za Busia-Eldoret-Malaba, Nairobi-Nakuru, Nairobi –Mombasa, Thika- Matu, Nakuru- Nyahururu kati ya zingine.

You can share this post!

Uume wa mwanamume aliyevamiwa Migori wapatikana TZ

KCB kuokoa pesa za mlipa ushuru ikununua National Bank

adminleo