• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
Hoteli yafungwa kwa kuwatoza wanaume ‘ushuru wa jinsia’

Hoteli yafungwa kwa kuwatoza wanaume ‘ushuru wa jinsia’

MASHIRIKA Na PETER MBURU

HOTELI moja ya Australia ambayo imekuwa ikitoza wanaume ‘ushuru wa jinsia ya uanaume’ kama mbinu ya kuleta usawa katika tofauti za malipo baina ya wanaume na wanawake ilifungwa Jumapili, baada ya kuhudumu miaka miwili.

Hoteli ya Handsome Her ambayo imekuwa ikiendeshwa na mwanaharakati Alex O’Brien tangu 2017 imekuwa ikiwatoza wateja wanaume ‘ushuru wa mwanamume’ kama mbinu ya kupigania usawa wa jinsia.

Hoteli hiyo imekuwa ikikosolewa na watu wengi kuwa inayoumiza jinsia moja, ikionekana kwa upana kama ya wanaume na wanawake wasagaji.

Katika ujumbe ambao ilitoa mitandaoni, Hndsome Her ilisema kuwa ushuru iliotoza wanaume umepingwa vikali mitandaoni.

“Jinsi dunia ilichukulia biashara yetu kutoza ushuru wa wanaume ilituonyesha kuwa hali si nzuri,” ujumbe huo ukasema.

Hoteli hiyo ilisema kuwa ilikuwa biashara ndogo iliyokuwa ikijaribu kupaza sauti kwa niaba ya wanawake lakini ikaishia kuwa iliyokuwa ikipigwa kote mitandaoni.

Habari kuhusu kufungwa kwake zilipokelewa kwa njia tofauti na umma, wanaume wengi wakizifurahia nao baadhi ya wanawake kushukuru kuwa ilijaribu kutetea haki zao.

You can share this post!

NOTRE DAME: Mtawa wa miaka 91 anauza ubikira kufadhili...

MAKOVO MBATHA: Wengi hawakutarajia ningefika hapa

adminleo