• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 6:55 AM
TAHARIRI: Kwa nini kila msimu mvua ilete maafa?

TAHARIRI: Kwa nini kila msimu mvua ilete maafa?

Wakazi wa mtaa wa South C, Nairobi wanavyohangaishwa na mafuriko kila kunaponyesha. Picha/ Maktaba

Na MHARIRI

MVUA iliyoanza kunyesha Alhamisi usiku katika maeno mengi ya nchi, imekuwa wakati ambapo imekuwa ikitarajiwa na wengi.

Kwa miezi kadhaa kumekuwa na kiangazi, na Shirika la Msalaba Mwekundu nchini limetangaza kwamba zaidi ya Wakenya milioni 3.4 wanahitaji chakula cha dharura cha msaada. Shirika hilo liliorodhesha kaunti kumi ambako wananchi na mifugo yao wamo kwenye hatari ya kufa kutokana na kiangazi.

Ukame umesababisha nyasi kukauka na hata akina mama wenye watoto wachanga kukosa maziwa ya kuwanyonyesha.

Kwa hivyo kulipoanza kunyesha, yalikuwa matarajio ya wengi kwamba mvua hii ingekuwa chanzo cha baraka kwa kila mmoja wetu.

Kinyume chake, baraka inayotokana kunyesha kwa mvua tayari imeanza kuwa ker, laana na kusababisha mahangaiko na hata mauti.

Kati ya Jumamosi usiku na jana alasiri, watu wanaotumia barabara kati ya Nairobi na Mombasa wamekuwa barabarani humo, baada ya ajali ndogo kutokea kwa sababu ya mvua. Msongamano mkubwa ulishuhudiwa, kiasi kwamba hakukuwa na anayeenda wala kurudi kwa zaidi ya saa 20.

Hali kama hiyo ilishuhudiwa katika jiji la Nairobi, ambapo maji yalifurika kwenye barabara na kuhatarisha maisha ya waendeshaji magari.

Katika maeneo mbalimbali, kufikia jana watu saba tayari walikuwa wameaga dunia kutokana na mafuriko.

Kinachoshangaza ni jinsi ambapo Kenya tuko na taasisi muhimu kama Idara ya Utabiri wa Hali ya Anga, ambayo ina wafanyikazi wanaolipwa ili kutoa ushauri kuhusu mambo kama haya.

Idara hiyo wiki jana ilitoa tahadhari na kueleza kwa urefu kuhusu hata maeneo ambako maafa hayo huenda yakatokea. Inashangaza kuwa hakuna hata mmoja wetu aliyechukulia ushauri huo kwa mazingatio yanayostahili.

Miji mingi bado haijazibua mitaro ya majitaka. Mashimo hayajazibwa na hakujawekwa mipango yoyote ya kuhakikisha kuwa, kuna usalama wa kutosha kwa wananchi walio katika kaunti zenye kukumbwa na radi za mara kwa mara.

Mambo haya yanafaa kuwa ya kuzingatiwa zaidi wakati huu, ikiwemo kuwashauri wananchi wahifadhi maji ya kutosha.

 

You can share this post!

Azomea mama kutaka aite wapenziwe ‘uncle’

OBARA: Ni aibu Kenya kuendelea kutegemea mvua pekee

adminleo