• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 6:50 PM
Migne aeleza sababu za kuwatema mastaa Were na Cheche

Migne aeleza sababu za kuwatema mastaa Were na Cheche

Na JOHN ASHIHUNDU
 
Kocha Sebastian Migne wa Harambee Stars amesema aliwatema Jesse Were na David ‘Cheche’ Ochieng kutokana na kudorora kwa fomu zao pamoja na mbinu atakazotumia kuwakabili wapinzani.
 
Hata hivyo, Cheche ameeleza anayesakatia AFC Leopards ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya Migne kumpuuza akisema ana haki ya kuchezea timu hiyo wakati fainali za Afcon zitakazofanyika nchini Misri kati ya Juni 21 na Julai 19.
 
Migne alitaja majina ya wachezaji 30 na kumuacha nje mshambuliaji Jesse Were ambaye hutegemewa na klabu ya Zesco United pamoja na Ochieng na badala yake kuwajumuisha kikosini Masoud Juma na John Avire, hatua ambayo ilizua mjadala mkubwa miongoni mwa wafuasi wa soka nchini.
 
“Nijuavyo, ni mshambuliaji bora kule Zambia lakini hapa nchini pia sisi tuko na mshambuliaji bora (Allan Wanga) kikosini. Leo hayuko kikosini lakini kesho nitamhitaji. Huenda akaimarika zaidi ili anivutie,” mkufunzi huyo alisema kuhusu hatua hiyo yake.
 
Kocha huyo wa zamani wa timu ya Jamhuri ya Congo kadhalika alimpuuza mlinzi Ochieng ambaye amekuwa akijumuishwa kwenye kikosi hicho kwa miaka saba iliyopita, mbali na kushiriki katika mechi zote za kufuzu kwa fainali hizo za bara.
 
Badala yake, kocha huyo amependelea kuwajumuisha mabeki chipukizi Joseph Okumu na Bernard Ochieng kikosini.
 
“Kwa hakika nimekasirishwa sana na uamuzi wa kocha kwa sababu naamini nilitakiwa kupewa nafasi nicheze fainali za bara,” Ochieng alisema.
 
“Ni jambo la kuudhi, lakini kawaida ni kocha aliye na uwezo wa kuunda timu. Nawatakia kila la heri, lakini sitaacha kuchezea timu ya taifa. Huenda wakati mmoja nikapata nafasi ya kusema zaidi kuhusu suala hili siku moja.”
 
Ochieng alijiunga na AFC Leopards kwa mkataba mfupi akitokea IF Brommapojkarna mwezi Machi mwaka huu tangu aanze likizo mwezi Desemba.
 
Nchini Misri, Harambee Stars imepangiwa katika kundi moja na Senegal ya Saidio Mane wa Liverpool na Rihard Mahrez pia wa klabu hiyo ya EPL ambaye barani atakuwa katika kikosi cha timu ya Algeria. Timu nyingine kwenye kundi hili ni Tanzania.
 
 

You can share this post!

Nyama ya mbuzi haina ladha tena, anawala vinyonga, kobe,...

Kocha mpya wa Malkia Strikers ashinikizwa kutetea ubingwa

adminleo