• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Uchukuzi wa BRT watengewa Sh5.5 bilioni

Uchukuzi wa BRT watengewa Sh5.5 bilioni

Na BERNARDINE MUTANU

Hazina ya Fedha imetenga Sh5.53 bilioni kutumiwa kujenga njia spesheli za kupitia magari makubwa ya uchukuzi wa umma katika juhudi za kumaliza msongamano Jijini Nairobi.

Fedha za maendeleo ya jiji katika bajeti ya mwaka huu wa kifedha ziliongezwa kutoka Sh18.79 bilioni hadi Sh24.33 bilioni ili kutekeleza mpango wa BRT.

Fedha hizo zitafaa zaidi mpango huo ambao ulikwama licha ya kutarajiwa kuwepo mwaka huu kutokana na ukosefu wa fedha za kutengeneza barabara na kununua mabasi makubwa kutoka Afrika Kusini.

Mfumo wa BRT umeundwa kwa lengo la kupunguza msongamano jijini na kuimarisha uchukuzi wa umma.

“Ongezeko hilo limetokana na ufadhili wa nje na mpango wa kubuni BRT,” ilisema Hazina ya Fedha katika bajeti ya ziada katika mwaka wa kifedha unaokamilika Juni.

Serikali imetangaza kuwa itajenga vivukio vya watumiaji barabara baada ya kilomita moja ili kuwawezesha abiria kuwa na uwezo wa kupata na kuchukua mabasi maalum ya BRT.

Kila basi linatarajiwa kuwa na uwezo wa kubeba watu 160, ambao watatumia kadi ili kulipa.

Mpango wa BRT utatekelezwa katika njia tano ambazo zimetengwa katika barabara kuu jijini.

Barabara hizo ni Thika Road, Jogoo Road, Mombasa Road, Lang’ata Road na Outering Road.

Mfumo wa BRT unatumiwa katika miji kadhaa Afrika, ukiwemo mji wa Dar-es-Salaam, Tanzania.

You can share this post!

KCB na National Bank kubuni benki yenye thamani ya Sh1...

Microsoft kushirikiana na vyuo vikuu kuvumisha teknolojia

adminleo