• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 4:36 PM
MKU yatenga Sh300 milioni kuendeleza ICT

MKU yatenga Sh300 milioni kuendeleza ICT

Na LAWRENCE  ONGARO

CHUO Kikuu cha Mount Kenya kimetenga Sh300 milioni kwa minajili ya kuendeleza teknolojia kupitia mpango wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

Mwenyekiti wa kamati ya chuo hicho Dkt Vincent Gichuru Gaitho, alisema mpango huo utanufaisha nchi nzima, bara la Afrika na hata ulimwenguni kwa jumla.

Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jana wakati wa kutia saini mkataba baina ya kampuni ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), na Chuo Kikuu cha Mount Kenya, mjini Thika katika chuo hicho.

Dkt Gaitho, alisema mpango huo wa uelewano utawapa wanafunzi mwelekeo wa kuelewa maswala ya teknolojia ya ICT kwa mafunzo hasa ya Microsoft.

Alisema habari na mawasiliano ni muhimu kwa uchumi wa kimaendeleo ambaye huboresha ajira na ushindani ya ujuzi.

Dkt Gaitho alisema kamati ya bodi ya chuo hicho imejitolea kuona ya kwamba maswala ya kidijitali yametiliwa maanani.

“Tumeona wageni wetu wakizuru eneo letu katika chuo hiki na pia wamejionea jinsi MKU imepiga hatua kielimu. Ninawashukuru wale wote waliofika kushuhudia mapatano yaliyofanyika. Tunapongeza ujumbe kutoka Microsoft, Tabarin, na Chuo Kikuu cha Mount Kenya hasa waliofanya mpango huo kuwa wa kufana,” alisema Dkt Gaitho.

Aliwahimiza wote waliohudhuria hafla hiyo kuzidi kukifadhili chuo hicho ili kuzidisha ushirikiano wao.

Teknolojia muhimu

Naibu Chansela wa chuo hicho Profesa Stanley Waudo alisema kwa wakati huu teknolojia ya ICT ni muhimu sana kwa kuendeleza masomo ya wanachuo.

“Masomo ya ICT ni muhimu kwa wanachuo kwa sababu ni rahisi kuwasiliana na yeyote aliye maeneo ya mbali. Kwa hivyo, ni vyema wanachuo kukumbatia teknolojia ya ICT,” alisema Prof Waudo.

Alisema mpango wa masomo ya mbali wa Open Distance Electronic Learning (ODEL) na Distance Institute Based Learning (DIBL) ni muhimu katika masomo ya kiteknolojia ya kisasa.

Alitaja kuwa kuna wanafunzi wapatao 6,027 katika kitengo cha ODEL) halafu 11,039 kwa upande wa DIBL.

Aliwapongeza wadau waliofanikisha mpango huo kupata mwongozo ufaao.

Hafla hiyo ilitiwa saini kati ya mkuu wa kitengo cha Middle East and Africa, Microsoft East Africa Bw Simone Outarra, na Naibu Chansela wa Chuo Kikuu cha Mount Kenya Profesa Stanley Waudo katika chuo hicho cha MKU mjini Thika.

Bw Outarra alisema ujumbe wa watu 60 utatumwa katika chuo hicho ili kuendeleza maswala ya ICT katika chuo hicho.

“Tunataka kuona wanafunzi wa chuo kikuu wakipata ujuzi wa kuwa wabunifu hasa katika kitengo wajuzi hasa katika kitengo cha ICT,” alisema Bw Outarra.

You can share this post!

Larry Mutunga: Anatumai kuwika katika soka, alenga kuiga...

BIMA: Wamiliki wa 14 Riverside kuvuna fidia ya Sh400m

adminleo