• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 6:47 AM
Watumizi wa mitandao ya kijamii Uganda kutozwa ushuru wa Sh100 kila siku

Watumizi wa mitandao ya kijamii Uganda kutozwa ushuru wa Sh100 kila siku

DAILY MONITOR na CHARLES WASONGA

WATUMIZI mitandao  ya kijamii nchini Uganda sasa watatozwa ushuru mpya ili kuzuia kile ambacho Rais Yoweri Museveni anataja kama “lugambo” (umbea).

Mitandao ya WhatsApp, Facebook, Twitter, Skype na Viber ni miongoni mwa mitandao inayolengwa kwani ndio hutumiwa na raia wengi nchini Uganda.

 Inadaiwa kuwa serikali ilichukua hatua hiyo kutokana na kile ambacho serikali inadai “ni tabia ya wananchi kuitumia mitandao hiyo kuikosoa serikali nila sababu yoyote.”

Bw Museveni pia analenga kuwatoza kodi zaidi wamiliki wa majengo ya kibiashara katika jitihada za kuimarisha mapato ya serikali kando na Sh50 bilioni ambazo hukusanywa kutoka kwa wamiliki wa nyumba kila mwaka.

Watumiaji mitandao ya kijamii walikashifu hatua ya serikali kuaza kutoza mitandao ya kijamii ushuru zaidi huku watetezi wa haki na viongozi wa upinzani wakidai hatua hiyo inahujumu haki za watu. Vile vile, wanalalamika kuwa ushuru zaidi ni mzigo kwa wananchi.

Katibu katika Wizara ya Fedha, Keith Muhakanizi na maafisa wa Ikulu ya Rais walithibitisha hatua hiyo.

Chini ya mpango huo, serikali ya Museveni inapania kukusanya Sh400 bilioni (za Uganda) na Sh1.4 trilioni (za Uganda) kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

“Hata hivyo, zitaweka ushuru mpya kwa watumiaji intaneti kwa shughuli za masomo na utafiti…. huduma hizo hazitakuwa zikitozwa ushuru wowote,” Bw Museveni akaandika.

“Hata hivyo, “olugambo” katika mitandao ya kijamii ( yaani maoni, matusi, kupiga soga) na matangazo  ya kampuni ya Google itatozwa kodi. Sijui ni nani mwingine anafaa kulipa ushuru kwa sababu tunahitaji rasilimali ili kukabiliana na matokeo ya “lugambo”.

Hata hivyo, Rais Museveni hakuelezea namna ambavyo “lugambo” (umbea) umeathiri juhudi za serikali za kukusanya mapato na rasimali nyingi za manufaa kwa ustawi wa nchini.

Museveni alisema chini ya mpango huo watumiaji mitandao ya WhatsApp, Skype, Viber, Twitter n.k watatozwa ada ya Sh100 kil siku. “Kwa jumla tutaweza kukusanya Sh400 bilioni zaidi kila mwezi,” akasema.

Kiongozi huyo alisema serikali yake ilichukua hatua hiyo pia baada ya kubainika kuwa raia wa Uganda hutumia simu zao kusakura mitandao ya kijamii badala ya kupiga simu za kawaida.

You can share this post!

Mke wa zamani wa Nelson Mandela, Winnie Madikizela afariki

Marufuku ya plastiki yamchochea Criticos kuwekeza upya kwa...

adminleo