• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:53 PM
Mzee Moi bado ajiona ndiye ‘rais wa Kenya’

Mzee Moi bado ajiona ndiye ‘rais wa Kenya’

Na MWANDISHI WETU

KATIKA mkutano wa kinara wa upinzani Raila Odinga na rais mstaafu Mzee Daniel Toroitich arap Moi Alhamisi, Wakenya wengi walishangazwa na picha iliyopigwa na kuwekwa mitandaoni ya wawili hao.

Kinachoshangaza katika picha hiyo ni kuwa Mzee Moi, katika picha iliyotundikwa ukutani sebuleni, ameweka picha yake na wala si ya Rais Uhuru Kenyatta, hasa ikizingatiwa kuwa yeye ni afisa wa zamani wa serikali.

Picha hiyo imewafanya Wakenya kuamini kuwa bado rais huyo wa zamani anaamini kuwa yeye ndiye rais wa Kenya hadi sasa.

Na kuna wale watakaokubaliana na mtazamo huo, hasa ikizingatiwa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2017, Rais Kenyatta alimtembelea Mzee Moi nyumbani kwake Kabarak, na kuzungumzia mambo kadhaa.

Pia ikumbukwe kuwa rais huyo mstaafu ndiye alimfungulai njia ya siasa nchini hapo mwaka 2002, alipomtangaza hadharani kuwa mgombeaji wa uaris kwa tiketi ya chama cha KANU wakati upinzani uliungana kwa mara ya kwanza kwa chama cha NARC na kufanikiwa kuing’oa KANU mamlakani.

Baada ya kumtambulisha Uhuru Kenyatta kwa wapiga kura mwaka huo, miaka kumi baadaye alishinda kura ya urais hapo 2013, na tena 2017.

Wadau wa siasa nchini hukubaliana kuwa Mzee Moi ndiye ‘profesa’ halisi wa siasa kutokana na maamuzi aliyokuwa akifanya akiwa madarakani..

You can share this post!

‘Baba’ akutana na Mzee Moi

Wazito wageuzwa wepesi na Gor

adminleo