• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 7:55 PM
Debi ya Mashemeji yaahirishwa

Debi ya Mashemeji yaahirishwa

Na GEOFFREY ANENE

GOZI kati ya AFC Leopards na Gor Mahia almaarufu ‘Mashemeji derby’ limeahirishwa.

Taarifa kutoka kwa kampuni inayoendesha Ligi Kuu ya Kenya (KPL) inasema kwamba kamati kuu ya KPL ilifikia uamuzi huo baada ya kushauriana Mei 23, 2018.

“Uamuzi wa Jopo la Kutatua mizozo katika michezo (SDT) Mei 23, 2018 jioni unasisitiza mamlaka KPL ilipewa katika kandarasi kati ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) na KPL, kuendesha ligi, na kuipa KPL mamlaka ya kufanya uamuzi wa mwisho kuhusu swala hili.

“Baada ya kushauriana na kamati kuu ya KPL, tunathibitisha kwamba mechi kati ya AFC Leopards SC na Gor Mahia FC iliyoratibiwa kusakatwa uwanjani Bukhungu mnamo Mei 26, 2018 imeahirishwa.

Tarehe mpya na uwanja utakaotumiwa zitatangazwa juma lijalo baada ya kushauriana na wenyeji, AFC Leopards SC. Kampuni ya KPL itaendelea kuheshimu na kufuata sheria katika soka ya Kenya na kulinda heshima na sifa ya Ligi Kuu ya Kenya,” kampuni hiyo ilisema.

Gozi hili lilikuwa limesababisha uhasama kati ya FKF na Gor Mahia upande mmoja na KPL na AFC Leopards kwa upande mwingine.

FKF na Gor zilitaka mchuano huu mkubwa katika kalenda ya ligi ya Kenya uahirishwe kupisha mechi za kimataifa kati ya Harambee Stars na Swaziland (Mei 25) na pia Equatorial Guinea (Mei 28). Nazo KPL na Leopards zilitaka mechi iendelee kama ilivyopangwa Mei 26.

You can share this post!

BI TAIFA MEI 11, 2018

FKF: Hatutaongezea KPL kandarasi ya kuendesha ligi 2020

adminleo