• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 11:05 AM
Auawa kwa kuchelewesha kulipa deni la Sh100

Auawa kwa kuchelewesha kulipa deni la Sh100

Na JADSON GICHANA

Biwi la simanzi lilitanda katika kijiji cha Randani, eneo la Kenyenya, Kaunti ya Kisii baada ya mwanamume kuua mwenzake kwa kukosa kumpa mgao wake wa Sh100 wa pesa walizolipwa baada ya kufanya kibarua.

Wakazi walisema kuwa James Karori mwenye umri wa miaka 22, aliuawa Jumapili asubuhi na Donald Onyango kwa upanga.

Baada ya kutekeleza kitendo hicho, mshukiwa alitoroka na wanakijiji  waliokuwa na hamaki  wakachoma boma lake.

Habari zilisema Marehemu Karori alikuwa miongoni mwa wanaume tisa ambao walipewa kandarasi na mzee mmoja ili kuhamisha paa la nyumba hadi nyumba nyingine mpya na wakalipwa Sh1,000 kugawanya kwa usawa akiwemo mshukiwa.

Kulingana na majirani, marehemu aliwapatia wengine Sh800 na akaendela kutafuta chenji ili aweze kumlipa mshukiwa, hali ambayo ilimkasirisha Onyango kwa kuwa muda wa saa 12 baadaye, hakuwa amempatia.

“Vijana hawa tisa walipewa kazi na mzee mmoja ya kuhamisha paa la nyumba hadi nyumba nyingine ambayo alijenga na akawapatia Sh1,000 wagawane.

Lakini Karori alienda kutafuta chenji na alipata 800 na kumueleza Onyango asuburi. Bw Karori alienda nyumbani kwao akalala nazo ndipo jirani yake akakasirika na kumuua kwa upanga,” Bw Joshua Kiomeri alieleza.

OCPD wa eneo hilo, Bw Isaac Thuranera alisema polisi wanaendela kumsaka mshukiwa huyo ambaye alitoroka kutoka eneo la Kisii.

 

You can share this post!

Wetang’ula atisha kutoboa siri zote za Raila Odinga

Korti yaruhusu serikali kujenga nyumba 7,000

adminleo