• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 12:58 PM
USALAMA SHULENI: Kamati ya Elimu yataka CCTV ziwekwe kuzima unajisi

USALAMA SHULENI: Kamati ya Elimu yataka CCTV ziwekwe kuzima unajisi

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kuhusu Elimu Julius Melly (kati) akiongoza wenzake kuhutubia wanahabari kuhusu suala la utovu wa usalama katika shule za umma. Hapa ni katika Majengo ya Bunge, Juni 5, 2018. Picha/ Charles Wasonga

Na CHARLES WASONGA

KAMATI ya Bunge kuhusu Elimu imeitaka serikali kupitia Wizara ya Elimu kuanzisha mikakati mipya ya kudhibiti usalama katika shule za humu nchini.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Bw Julius Melly wabunge wanachama wa kamati hiyo wanaitaka wizara ya elimu kununua vifaa vya usalama kama vile mitambo ya CCTV kando na kuajiri walinzi waliohitimu katika shule za umma, haswa zile za mabweni.

“Wizara ya Elimu inafaa kubadili mikakati yake ya kudumisha usalama katika shule zetu kwa sababu wahalifu nao wamebadili mbinu zao. Kwa hivyo kando kuajiri walinzi shule, Wizara ya Elimu inafaa kuweka mitambo ya kisasa kama vile CCTV ambayo itarekodi matukio yote shule,” akasema Bw Melly Jumanne kwenye kikao na wanahabari katika majengo ya bunge.

Bw Melly alinukuu Katiba, sehemu ya sheria ya Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) na sheria ya Elimu ya Msingi zinazosema kuwa wanafunzi hawapasi kupitia aina yoyote ya dhuluma wakiwa shule, akisema wizara ya elimu kuhakikisha kuwa sheria hizo zimezingatiwa.

“Kwa hivyo, waziri wa elimu Amina Mohamed, Katibu wa wizara, wakurugenzi wa elimu katika ngazi zote, na haswa walimu wakuu, wanapaswa kuhakikisha kuwa sheria hizi zinatekelezwa kwa manufaa ya wanafunzi,”akasema akiongeza kuwa masomo hayawezi kunawiri vizuri katika mazingira ya utovu wa usalama.

Kamati hiyo ilaani kisa cha unajisi wa wanafunzi katika Shule ya Upili ya Moi Girls na kuwata polisi na idara husika za upelelezi kuharakisha uchunguzi kuhusu kisa hicho.

You can share this post!

Kanze Dena ateuliwa Naibu Msemaji wa Ikulu

Wabunge wamtaka Rais kuwasimamisha kazi mawaziri na...

adminleo