• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 4:50 PM
Gavana akataza maafisa kuongea na wanahabari

Gavana akataza maafisa kuongea na wanahabari

Na Oscar Kakai

GAVANA wa Kaunti ya Pokot Magharibi, Prof John Lonyangapuo amepiga marufuku vyombo vya habari kuangazia masuala ya kaunti hiyo bila idhini yake.

Jana, Prof Lonyangapuo aliwaonya maafisa wa kaunti yake dhidi ya kutoa habari kwa waandishi wa habari bila kibali cha ofisi yake.

“Sitakubali huu mtindo wa watu kuhutubia wanahabari kuhusu masuala ya kaunti bila kuidhinishwa nami, seneta au kamishna wa kaunti,” alisema Prof Lonyangapuo.

Haya yanajiri baada ya vyombo vya habari kuangazia malalamiko ya wakazi kuhusu Naibu Gavana Dkt Nicholas Otudonyang kuwa nje ya nchi kwa muda mrefu.

Alisema kuwa vyombo vya habari vimeangazia vibaya kaunti hiyo na sasa wameanza mchakato wa kutengeneza jina la kaunti hiyo.

Lakini suala hilo halikuwafurahisha baadhi ya viongozi wa kaunti hiyo ambao wanasema hii ni mojawapo ya njia ya kuzima kazi ya vyombo vya habari.

You can share this post!

MCA watupwa nje ya basi kwa kudai marupurupu njiani

Sodo zatajwa sababu ya mimba za mapema Pwani

adminleo