• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 AM
Mifupa ya watoto 56 waliotolewa kafara yafukuliwa

Mifupa ya watoto 56 waliotolewa kafara yafukuliwa

Na MASHIRIKA na VALENTINE OBARA

HUANCHACO, PERU

WATAFITI wa mambo ya kale wamefukua mifupa ya watoto 56 wanaoaminika walitolewa kafara Peru.

Inaaminika watoto hao waliuawa kwenye kafara iliyolenga kuomba miungu wasitishe mafuriko yaliyokuwa yakisababishwa na mvua la El Nino karibu miaka 600 iliyopita katika Wilaya ya Huanchaco, mjini Trujillo kaskazini mashariki mwa Peru.

Watafiti waliohojiwa na mashirika ya habari walisema uchunguzi wao umebainisha kwamba eneo ambako mifupa ya watoto hao ilipatikana lilikuwa la kutoa kafara za binadamu katika enzi za kale.

Ripoti zinasema kwamba watoto hao walikuwa wenye umri wa kati ya miaka sita hadi 14 na walizikwa kati ya mwaka wa 1,200 AD na 1,400 AD.

Ingawa haikubainika wazi jinsi walivyouawa, ilipatikana kwamba miili hiyo ilikuwa imefungwa kwenye vitambaa kuashiria kwamba kulikuwa na maandalizi fulani kabla watolewe kafara.

Mmoja wa watafiti, Prof John Verano, alinukuliwa kusema uchunguzi ulionyesha kuwa watoto hao walikuwa wenye afya njema walipofariki.

Ilisemekana ufichuzi huu ni iadi kubwa zaidi ya kafara za binadamu kuwahi kuonekana katika historia.

You can share this post!

Nilimuua mume wangu kwa kutesa paka wangu, akiri mwanamke

Kidosho apaka mboni ya macho rangi na kupasua ulimi kama wa...

adminleo