• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 2:18 PM
KCB washindwa kutwaa ubingwa wa voliboli Rwanda

KCB washindwa kutwaa ubingwa wa voliboli Rwanda

Na GEOFFREY ANENE

MABINGWA wa Afrika mwaka 2006, KCB walikamilisha Voliboli ya Rwanda Genocide Memorial katika nafasi ya pili baada ya kunyukwa seti 3-1 na Chuo Kikuu cha Nkumba kutoka Uganda jijini Kigali, Jumapili usiku.

Gazeti la New Times nchini Rwanda limeripoti kwamba KCB kutoka Kenya ilianza fainali kwa kunyakua seti ya kwanza 25-23, lakini ikasalimu amri katika seti tatu zilizofuata 25-15, 25-22 na 25-19 na kupoteza mechi hiyo.

Vipusa wa kocha Vernon Khainga walikuwa na matumaini makubwa ya kutwaa taji baada ya kuzima mabingwa wa mwaka 2017 APR kwa seti 3-0 katika nusu-fainali. Hata hivyo, Nkumba, ambayo ililemea Rwanda Revenue Authority 3-2 katika nusu-fainali, iliizima katika fainali baada ya kuonyesha mchezo wa hali ya juu.

Mabingwa walizawadiwa Sh115,967, nambari mbili Sh69,547 nao nambari tatu wakaridhika na Sh46,365. KCB ni timu pekee kutoka Kenya iliyoshiriki voliboli makala ya mwaka 2018.

Wenyeji Gisagara walishinda kitengo cha wanaume baada ya kulima Rwanda Energy kwa seti 3-0.

You can share this post!

KUPUNGUZA AJALI: Serikali yaanza kupanua barabara Salgaa na...

Kipa apigwa marufuku kwa kudaganya ana jeraha ili kocha...

adminleo