• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
Wateja wa Equity walemewa kulipa mikopo

Wateja wa Equity walemewa kulipa mikopo

Na BERNARDINE MUTANU

BENKI ya Equity imepungukiwa na mapato kutokana na kiwango kikubwa cha wateja, hasa wamiliki wa biashara ndogo, ambao wameshindwa kulipa mikopo.

Akiongea wakati wa kutoa ripoti ya ilivyofanya benki hiyo katika muda wa miezi sita ya mwanzo 2018 Alhamisi, Mkurugenzi Mkuu wa Equity Dkt James Mwangi alisema kiwango cha wamiliki wa biashara ndogo ambao hawajalipa mikopo, pamoja na kudhibitiwa kwa viwango vya riba kumeifanya benki hiyo kutafuta mbinu zingine.

Kulingana na benki hiyo, hali ya kutolipa mikopo inatokana na watoaji wa mizigo na bidhaa kutolipwa na serikali.

“Tunaelewa kuwa wafanyibiashara wadogo wanatatizika kufanikisha wajibu wao katika kulipa mikopo kwa sababu ya kulipwa wakiwa wamecheleweshwa na serikali za kaunti na serikali kuu. Kiwango cha mikopo ambayo hailipwi ni asilimia 12.1. Kiwango hicho ni cha juu sana,” alisema Mwangi.

Mkurugenzi huyo alielezea matumaini yake kwamba hali itaimarika hasa kutokana na mandhari ya kisiasa nchini, baada ya muda mrefu wa kisiasa nchini.

You can share this post!

Shilingi ya Kenya yaimarika zaidi

Agosti 21 yatangazwa sikukuu ya Idd-ul-Azha

adminleo