• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM

Washindi wa insha za ‘Taifa Leo’ watuzwa Sh50,000 kila mmoja

NA CHRIS ADUNGO WANAFUNZI sita walioibuka mabingwa wa kitaifa katika ‘Shindano la Uandishi wa Insha za Taifa Leo’ katika miaka ya kiakademia ya 2021 hadi 2022 walituzwa karo ya Sh50,000 kila mmoja hapo jana katika jumba la Nation Centre, Nairobi. MwanaIddi Majaliwa wa Mtondia Highway Trinity (Tezo, Kilifi), Alvine Juma Oduor wa Lukonyi Boys (Matayos, […]

Mabingwa wa insha Pwani wapimana ujuzi

NA JURGEN NAMBEKA WANAFUNZI wa shule za upili na za msingi walioibuka waandishi bora wa insha za shindano la Taifa Leo kipindi cha mwaka wa 2021 hadi 2022 Pwani, hapo jana walikongamana jijini Mombasa kushiriki raundi ya mwisho ya mashindano ya kieneo. Mabingwa hao waliotoka katika kaunti zote sita za Pwani walishiriki uandishi wa insha, […]

NGUVU ZA HOJA: Baraza la Mtihani lafaa kutahini uandishi wa Insha katika CBC

NA PROF JOHN KOBIA TATHMINI ya tamati ya kwanza ya Mtaala wa Umilisi kwa wanafunzi wa gredi ya sita yaani Kenya Primary School Education Assessment (KPSEA) inatarajiwa kuandaliwa na Baraza la Mitihani la Kenya (KNEC) mwishoni mwa mwaka huu. Tathmini hii itachukua asilimia 40 huku tathmini endelevu ambayo imekuwa ikiendelea ichukue asilimia 60 katika masomo […]

Inshallah nchi yetu iwe na amani zaidi mwaka 2022

Na WALLAH BIN WALLAH KWANZA kabisa tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa rehema zake za kuwa nasi tangu mwanzo wa mwaka 2021 hadi tukafika tulipofika leo. Jina lake lihimidiwe! Pili tuwaombee wenzetu tulioanza nao safari pamoja lakini kwa mapenzi ya Mola Muumba wetu wakaitikia wito usiopingika! Roho zao zihifadhiwe mahali pema peponi! Amina! Safari ya maisha ni […]

Mwanataekwondo Ogallo ashinda uandishi wa insha ya Olimpiki Kenya

Na GEOFFREY ANENE NYOTA Faith Ogallo si mchache tu katika mchezo wa taekwondo! Ogallo, ambaye atawakilisha Kenya kwenye Olimpiki katika mchezo wa taekwondo mjini Tokyo, Japan, ameshinda mashindano ya siku ya Olimpiki (kitengo cha kuandika insha) mnamo Juni 30. Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki Kenya (NOC-K) imetangaza kuwa mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Kibabii […]

Wakenya waendea medali za dhahabu ndondi za Ukanda wa Tatu jijini Kinshasa

Na GEOFFREY ANENE MASHINDANO ya masumbwi ya Afrika ya ukanda wa tatu yatafikia kilele mjini Kinshasa hii leo Ijumaa, ambapo Wakenya watano wanawinda dhahabu. Christine Ongare (uzani wa kilo 51), Nick ‘Commander’ Okoth (kilo 57) na Elly Ajowi (zaidi ya kilo 91), ambao wamefuzu kushiriki Michezo ya Olimpiki baadaye mwaka huu, wako katika fainali ya […]

Matokeo mseto kwa mabondia wa Kenya jijini Kinshasa, Commander azidi kutisha

Na GEOFFREY ANENE WAKENYA Nick Okoth, Joshua Wasike na George Cosby Ouma walivuna ushindi muhimu kwenye mashindano ya masumbwi ya Afrika ya ukanda wa tatu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jumanne. David Karanja na Martin Aluoch pia walipata ushindi kwenye mashindano hayo yanayotumia mfumo wa mzunguko, lakini bila jasho baada ya kupewa ushindi wa […]

Droo ya masumbwi ya Kinshasa yafanywa mataifa manne yakijiondoa kwa sababu ya masharti makali ya corona

Na GEOFFREY ANENE MATAIFA manne yamejiondoa kwenye mashindano ya masumbwi ya Afrika ya ukanda wa tatu yatakayoanza jijini Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mnamo Machi 22. Uganda, Equatorial Guinea, Gabon na Morocco zimejiondoa dakika ya mwisho kutokana na masharti magumu ya usafiri wakati huu wa janga la virusi vya corona. Mashindano hayo sasa […]