• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 4:28 PM

MALENGA WA WIKI: Kifo cha Sudi Kigamba ni pigo kwa tasnia ya ushairi na taaluma ya Kiswahili

Na HASSAN MUCHAI MAREHEMU Al- Haji Sudi Kigamba aliyejulikana kwa lakabu ya ‘’Mwanamrima’’ alikuwa na mambo mawili aliyotaka kutimiza pindi angetua nchini Kenya mwezi Machi au Aprili mwaka 2021. Kupitia ujumbe wake ulionukuliwa Agosti 16, 2019, Marehemu alitaka kuyakusanya mashairi ya marehemu Mwalim Mbega akiwa na nia ya kuandika wasifu wake. Kilichomkwaza sana kutimiza azma […]

Simanzi gwiji wa ushairi akifariki

JUMA NAMLOLA na CHRIS ADUNGO WAPENZI wa Kiswahili wamepata pigo baada ya mshairi mkongwe Abdalla Mwasimba kuaga dunia hapo Jumatano akiwa na umri wa miaka 83. Jamaa na marafiki waliofika katika makaburi ya Waislamu ya Kariokor, Nairobi, walimmiminia sifa Mzee Mwasimba, ambaye ni Mkenya wa kwanza kuwahi kughani mashairi redioni. Mtindo wake wa kughani ulivutia […]

Pigo kwa ushairi mlumbi maarufu Shamte akifariki

MISHI GONGO na HASSAN MUCHAI ULIMWENGU wa ushairi unaomboleza kifo cha mshairi mkongwe Abdallah Ali Shamte (pichani kushoto), aliyejulikana kwa lakabu “Mtumwa wa Mungu.” Alifariki Jumapili usiku nyumbani kwake mjini Mombasa. Mzee Shamte amekuwa akiugua kwa muda hali iliyomzuia kutembea kwa mwendo mrefu. Marehemu aliswaliwa katika msikiti wa Kwa-Shibu na kuzikwa maziara ya Sargoi jana […]

KAULI YA MATUNDURA: Mgogoro wa ushairi wa Kiswahili ulivyomtia matatani mtaalamu Mugyabuso Mulokozi

Na BITUGI MATUNDURA MNAMO 2017, nilifanya utafiti kuhusu ‘mgogoro wa ushairi wa Kiswahili’ uliozuka mnamo miaka ya 1960. Mgogoro huo miongoni mwa wataalamu wa Kiswahili ulichochewa na masuala mawili. Kwanza, utata kuhusu maana ya ushairi kwa jumla. Iliki, maana ya ushairi wa Kiswahili. Mgogoro huo ulizua mapote mawili yaliyokinzana. Pote la kwanza lilikuwa na wanamapokeo […]

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Nafasi ya ushairi katika uwasilishaji wa Fasihi

Na CHRIS ADUNGO USHAIRI wa Kiswahili una dhima kubwa mno katika Fasihi Simulizi na Andishi. Ushairi umetumiwa sana katika tanzu mbalimbali za fasihi kwa sababu mbalimbali. Nyimbo kwa mfano zimetumiwa sana katika kuandika na kuwasilisha maudhui ya riwaya, tamthilia, novela na hata hadithi fupi. Zaidi ya mambo mengine, matumizi hayo yana dhima ya kutambulisha wahusika, […]

USHAIRI WENU: Mamba wala nchi

WAPO wengine wanyama, nyumbani hata porini,Wale walo na unyama, wasoyala na majani,Kesha fika kwa mapema, kututia matatani,Nivusheni baharini, penye mamba wala nchi.Keshawaona kitambo, wameasi ya adhimu,Wamo kutupiga kumbo, na kusitiri ilimu,Daima si haijambo, tumepoteza fahamu,Nivusheni baharini, penye mamba wala nchi.Wapo nchini hakika, wamepaka yao sura,Wajulikana kihulka, walaji hongo ya chira,Wasopenda ushirika, wenye nyoyo za ngawira,Nivusheni […]

USHAIRI WENU: Mtima wangu tulia

Mtima wangu tulia Mtima wangu sikia, jifunze kuvumilia,Mtima wangu tulia, machungu yapokujia,Mtima wangu umia, lakini usijelia,Mtima wangu tulia, jifunze kuvumilia.Mtima wangu sikiza, koma kuniaibisha,Komata kuutangaza, udhaifu wa maisha,Mwili wangu kuuguza, maumivu yanachusha,Mtima wangu tulia, jifunze kuvumilia.Mtima wangu hakika, umeniponza yakini,Ukiitwa waitika, yeyote wamuamini,Ukipendwa wapendeka, bila ya kuwa makini,Mtima wangu tulia, jifunze kuvumilia.Mtima wangu kwanini, usiwe […]

USHAIRI WENU JUMAMOSI, MACHI 2, 2019

Na MKUSANYAJI WA MASHAIRI HAYA ni mashairi ambayo yamechapishwa kwenye gazeti la Taifa Leo toleo la Jumamosi, Machi 2, 2019.   MWALIMU KAMA MWALIMU Mwalimu kweli mwalimu, nampongeza mwalimu, Yeye ni mtu muhimu, mwalimu tumuheshimu, Ana mengi majukumu, nawajuvya mfahamu, Hakuna kama mwalimu, sifaze ni nzima chungu.Hufunza mwenendo mwema, wanafunzi darasani, Wote wawe na heshima, […]

USHAIRI WENU: Kazi nitazochapa

Na DOTTO RANGIMOTO YA Rabi kutoka kapa, mjawo ninaogopa,Kazi nitakazochapa, waja wasije zikopa,Kisha zisikome hapa, zifike hadi Yuropa.Nilisema sina pupa, Mungu yupo atanipa,Iwe nyama ama fupa, kidumu au jipipa,Neno hili sitatupa, hini dhima nimejipa.Enda yangu nyapanyapa, taratibu ninadupa,Nazidi kuchapa lapa, Mola usije nitupa,Kiapo leo naapa, mpaka sitauchupa.Tamati kunao papa, Rabi siwezi wakwepa,Kwa hivi wanavyotapa, dagaa […]

SHAIRI: Ushairi tujifunze, tupate kuumaizi

Na KULEI SEREM Istilahi za shairi, zimepangwa kwa mpororo,  Mishororo ni mistari, kama kamba na nyororo, Wengi wanatahadhari, ila ni jambo jororo, Ushairi tujifunze, tupate kuumaizi. Mistari ina vipande, wahitaji kumaizi, Sikizeni chondechonde, mambo ni ya waziwazi, Ukwapi kwanza kipande, utao na mwandamizi, Ushairi tujifunze, tupate kuumaizi. Sitasahau ukingo, ndicho kipande cha mwisho, Hili ni […]