17/07/2018

Kipa Okello arudi kuchezea Mathare Utd

Na JOHN ASHIHUNDU

Kipa David Okello amejiunga tena na klabu ya Mathare United baada ya kuagana na Tusker.

Mlinda lango huyo alithibitisha jana kuwa mchezaji wa pili kujiunga na Mathare wakati huu wa wachezaji kuhama.

Okello amerejea kuchukua nafasi ya Wycliffe Kasaya ambaye amehamia Sofapaka FC.

Atasaidiana na Robert ‘Boban’ Mboya, Emmanuel Otieno na Job Ochieng.

“Nafurahia kurejea nyumbani. Mazingara ni sawa kwa sababu niliwahi kucheza na baadhi ya wachezaji walio klabuni kwa sasa. Bila shaka mashabiki watatarajia makubwa kutoka kwangu na niko tayari kwa upinzani wowote kutoka kwa makipa wenzangu. Mathare ni klabu nzuri iliyo na hamu kuu ya kupata mafanikio,” Okello alisema kupitia kwa mtandao wa klabu hiyo ya kocha Francis Kimanzi ambao wako katika nafasi ya pili jedwalini, nyuma ya Gor Mahia.

“K’Ogalo wanaongoza msimamo, lakini tutaendelea kuwafukuza hadi dakika ya mwisho. Kumbuka mechi 10 zilizobaki ni nyingi,” alisema Okello.

Habari zinazohusiana na hii