25/06/2018

Ndani kwa kufungia mtoto na paka 39 ndani ya gari

Na MASHIRIKA na VALENTINE OBARA 

OAKDALE, AMERIKA

POLISI walimkamata mwanamke aliyemfungia mtoto wake na paka wapatao 39 kwenye sehemu ya gari ya kubebea mizigo.

Ripoti za mashirika ya habari zinasema polisi waliarifiwa na wakazi wa mtaa ulio mjini Oakdale, California kuhusu mwanamke aliyekuwa na paka wengi waliodhaniwa kuwa wagonjwa.

Wakati polisi walipowasili kuchunguza kilichokuwa kikiendelea, walimkuta mwanamke huyo aliyetambuliwa kama Heidi Gusman, 51, nyumbani kwake.

Uchunguzi wao uliwaelekeza kwa gari ambapo sauti za migongano zilikuwa zikisikika. Walipofungua ndipo walipata mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 11 akiwa amefungiwa pamoja nap aka 39.

Kwa mujibu wa mashirika ya habari, mtoto na wanyama hao walikuwa wadhaifu hasa kutokana na kuwa California huwa ni eneo lenye joto jingi kwa viumbe hao kufungiwa namna hiyo.

Ilisemekana Gusman alitupwa kizuizini na anatarajiwa kushtakiwa kwa kutesa mtoto na wanyama, huku mtoto wake akipelekwa katika kituo cha ulezi wa watoto waliotelekezwa.

Habari zinazohusiana na hii