• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 9:50 AM
Barcelona, Bayern Munich na Inter Milan watiwa katika kundi gumu UEFA

Barcelona, Bayern Munich na Inter Milan watiwa katika kundi gumu UEFA

Na MASHIRIKA

LIVERPOOL watakutana na Rangers ya Scotland katika hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu huu huku nyota Erling Haaland akitarajiwa kumenyana na waajiri wake wa zamani baada ya Manchester City kutiwa katika zizi moja na Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Wafalme wa Ligi Kuu ya Scotland, Celtic, wametiwa katika kundi moja na Chelsea, AC Milan na washikilizi wa taji la UEFA, Real Madrid.

Eintracht Frankfurt ambao watanogesha soka ya UEFA kwa mara ya kwanza katika historia, wamepangwa katika Kundi moja na Tottenham Hotspur.

Bayern Munich, Barcelona na Inter Milan wametiwa katika Kundi C pamoja na Viktoria Plzen kutoka Jamhuri ya Czech.

Mechi za hatua ya makundi zimeratibiwa kusakatwa kati ya Septemba 6 na Novemba 2, 2022. Fainali ya UEFA msimu huu itachezewa uwanjani Ataturk Olympic jijini Istanbul, Uturuki mnamo Juni 10, 2023.

DROO YA UEFA:

KUNDI A: Ajax, Liverpool, Napoli, Rangers

KUNDI B: Porto, Atletico Madrid, Bayer Leverkusen, Club Bruges

KUNDI C: Bayern Munich, Barcelona, Inter Milan, Viktoria Plzen

KUNDI D: Eintracht Frankfurt, Tottenham, Sporting Lisbon, Marseille

KUNDI E: AC Milan, Chelsea, RB Salzburg, Dinamo Zagreb

KUNDI F: Real Madrid, RB Leipzig, Shakhtar Donetsk, Celtic

KUNDI G: Manchester City, Sevilla, Borussia Dortmund, FC Copenhagen

KUNDI H: Paris St-Germain, Juventus, Benfica, Maccabi Haifa

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Wabunge wapya wafika bungeni kuelewa mazingira ya kazi

KCB FC yakung’uta Bidco, Eastlanders kirafiki Ligi Kuu...

T L