• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 1:51 PM
Botswana kuanza kufundisha somo la Kiswahili katika shule

Botswana kuanza kufundisha somo la Kiswahili katika shule

Na XINHUA

BOTSWANA imeingia kwenye orodha ya mataifa ya Afrika ambayo yametangaza kuwa yataanza kufundisha Kiswahili katika shule.

Akizungumza katika kongamano mjini Francistown, nchini Botswana, Waziri wa Elimu ya Msingi nchini humo, Fidelis Molao, alisema Kiswahili kitaanza kufunzwa katika shule zake karibuni.

“Tunataka watoto na raia wa nchi hii waifahamu lugha ambayo inaendelea kukua kwa kasi ya Kiswahili. Mataifa yaliyo kwenye eneo la Maziwa Makuu yanaendelea kuwa na ushawishi mkubwa wa kiuchumi na hatuwezi kushirikiana nao bila ya kuifahamu lugha yao,” akasema.

Mpango huo wa kufunza Kiswahili unaonekana kufuata mkondo wa Afrika Kusini ambako Kiswahili kinafunzwa kama lugha ya ziada baada ya Kiingereza na Kiafrikana.

Mbali na Kenya na Tanzania, Kiswahili kinazungumzwa pia DRC, Rwanda, Uganda, Kaskazini mwa Malawi, Msumbiji, Zambia, Madagascar, Ethiopia na Comorros.

Pia kinafunzwa katika vyuo vikuu vingi ulimwenguni.

nchini Ujerumani, Uingereza, Canada, Urusi, China, Australia, India kati ya mataifa mengine mengi.

You can share this post!

Wanasiasa wachochezi kukabiliwa vikali

‘Nchi nyingi hazithamini usalama wa wahamiaji na watafuta...