• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 9:35 PM
Data: Serikali yaipiga breki Worldcoin

Data: Serikali yaipiga breki Worldcoin

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imepiga marufuku harakati za Worldcoin, kampuni ambayo imekuwa ikiendesha ukusanyaji wa data za Wakenya kutumia mitambo ya kumilika mboni za macho.

Kampuni huyo ya sarafu ya mtandaoni inayotumia teknolojia ya ‘blockchain’ imekuwa ikimtuza kila anayejitokeza kusajiliwa kwa kumtuza Sh7,000.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Waziri wa Usalama wa Ndani Profesa Kithure Kindiki amesema Jumatano kwamba kampuni hiyo ni sharti itoe maelezo ya namna inavyolenga kutumia data inazokusanya.

“Vitengo vya usalama, mashirika ya kifedha na mamlaka ya kuhifadhi data za Wakenya wameanzisha uchunguzi kubaini uhalali na uzingativu wa sheria kwenye shughuli inayoendeshwa na kundi hilo na usalama wa data zinazokusanywa pamoja na jinsi zitahifadhiwa ziwe salama,” amesema waziri Kindiki.

Aidha Kindiki ameonya yeyote anayefadhili au kujihusisha kwa njia yoyote na ukusanyaji wa data unaokiuka sheria.

  • Tags

You can share this post!

Mzaha mzaha huzaa talanta

Wakulima waonywa kuhusu kemikali nyingi

T L