• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 11:05 AM
Duale aapa kupinga Mswada wa miungano ya kisiasa

Duale aapa kupinga Mswada wa miungano ya kisiasa

Na KENYA NEWS AGENCY

MBUNGE wa Garissa Mjini Aden Duale (pichani) ameapa kuongoza wabunge wanaomuunga mkono Naibu Rais William Ruto, kupinga mabadiliko katika mswada wa vyama vya kisiasa utakaojadiliwa bungeni leo.

Akizungumza na wanahabari katika makazi yake mjini Garissa, Duale, ambaye alikuwa Kiongozi wa Wengi Bunge la Kitaifa, alisema mswada huo unasukumwa na watu wanaotaka kurudisha nyuma demokrasia na usimamizi unaofurahiwa na vyama vya kisiasa.

Wiki jana, Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi alitoa ilani ya kikao maalumu cha bunge Jumanne na leo kujadili masuala kadhaa ukiwemo mswada itakaoruhusu uundwaji wa miungano kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

“Baadhi ya mapendekezo yanakiuka haki inavyoeleza Katiba ya 2010. Tutaupinga mswada huo kortini iwapo utapitishwa na bunge,” alisema Bw Duale.“Mswada huo unaingilia sheria ya vyama vya kisiasa na kwa mara ya kwanza unabadilisha vifungu vya 2, 5 na 8 d.

Kwa hivyo, maelezo yote kuhusu vyama vya kisiasa yanabadilishwa,” aliongeza.Alisema mswada huo unaanzisha mahitaji magumu katika mchujo wa vyama vya kisiasa.

You can share this post!

Waliofariki kimbungani Ufilipino sasa wafika 375

Raila atema washauri wa jadi, ateua wapya

T L