• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 6:55 PM
EAC sasa yaungana kumuunga mkono Amina Mohamed kuwa kinara wa WTO

EAC sasa yaungana kumuunga mkono Amina Mohamed kuwa kinara wa WTO

NA FAUSTINE NGILA

NI RASMI kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) sasa inampigia upatu Waziri wa Michezo Amina Mohamed kuwa kinara wa Shirika la Biashara Duniani (WTO).

Tangazo hilo lilitokea Jumapili, siku mbili kabla ya shirika hilo kutangaza orodha ya mwisho ya wawaniaji wawili katika raundi ya mwisho ya kinyang’anyiro hicho.

Waziri wa Masuala ya Kigeni wa Rwanda Vincent Biruta, ambaye ndiye mwenyekiti wa sasa wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Masharii alisema kuwa Bi Mohamed amepata uungwaji mkono kutoka kwa mataifa yote ya EAC kufuatia ombi la Rais Paul Kagame.

“Ombi hapa limetolewa kumuunga mkono mwaniaji kutoka Kenya kwa wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa WTO. Ningependa kuwaarifu kuwa Balozi Amina C Mohamed amekubalika kama mwaniaji anayefaa zaidi na EAC,” Bw Biruta aliandikia mataifa ya Kenya, Burundi, Uganda, Tanzania na Sudan Kusini.

Bi Mohamed ni miongoni mwa wawaniaji wengine watano wanaomenyania hatua inayofuata ya mchujo itakayotangazwa Jumanne.

Wapinzani wake ni Dkt Ngozi Okonjo-Iweala wa Nigeria, Bi Yoo Myung-hee wa Korea Kusini, Bw Mohammad Maziad Al-Tuwaijri wa Saudi Arabia na Dkt Liam Fox wa Uingereza.

You can share this post!

SIHA NA LISHE: Vyakula unavyotakiwa kula kwa tahadhari au...

Ruto ana hasira za mkizi, hafai kuingia Ikulu – Junet...