• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 4:31 PM
FASIHI SIMULIZI: Fasili, sifa, dhima na aina za ngomezi

FASIHI SIMULIZI: Fasili, sifa, dhima na aina za ngomezi

Ngomezi ni nini? (alama 2)

Ni sanaa/fasihi inayotumia ala za kimuziki kuwasilisha ujumbe kwa hadhira au jamii.

Fafanua sifa zozote tano za ngomezi (alama 5)

Hutumia midundo mbalimbali ya ngoma/ala za muziki.

Huhitaji mtaalam wa ngoma.

Maana ya midundo mbalimbali hubadilika kutoka kwa jamii moja hadi nyingine. Ni vigumu kwa mgeni au jamii hasimu kutambua ujumbe wake.

Ngomezi ni fasihi simulizi kongwe zaidi.

Hutumika zaidi katika ulimwengu wa tatu/Afrika.

Hubadilika kutegemea na wakati; rununu kutoka kwa ngoma Toni au mipigo huwasilisha maneno/ujumbe maalum

Je, ngomezi ina umuhimu/dhima gani katika jamii yako? (alama 5)

Njia ya mawasiliano kwa jamii zisizojua kusoma.

Husaidia wanaokabiliwa na ugumu wa mawasiliano.

Kuharakisha mawasiliano katika masafa mafupi.

Kutoa taarifa kuhusu matukio fulani k.m. ndoa na kifo.

Husaidia kupitisha jumbe za dharura. Kutahadharisha wanajamii kuhusu tukio la hatari/dharura k.v. vita, gharika.

Kuficha siri kwa kuwasilisha ujumbe kwa njia iliyofumbwa.

Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wa jamii.

Namna ya kudhihirisha ufundi wa kutumia zana kama ngoma.

Kitambulisho cha jamii kwani kila jamii hupitisha ujumbe kwa mapigo tofauti.

Taja ngomezi zozote nne za kisasa (alama 2)

Milio ya rununu/simu

Filimbi michezoni/ya bawabu

Milio ya ambulensi/polisi

Kengele shuleni/mikutanoni

Honi za magari

Changamoto sita za ngomezi katika jamii ya sasa (alama 6)

Mwingiliano wa jamii mbalimbali unaosababisha kutofasiri ujumbe kwa njia moja inayotakikana.

Viwanda na majumba marefu kusababisha kutosikika kwa sauti au milio ya ngoma.

Njia nyingine za kisasa za mawasiliano zinazotumiwa kwa wingi na kwa wepesi.

Uhaba wa zana za kitamaduni kama baragumu na zumari zilizokuwa zinatumika.

Mabadiliko ya maisha kuleta ubinafsi na kusababisha wengi kutoitikia wito wa vyombo.

Uhaba wa wataalamu/wajuzi wa ala za kimuziki zinzotumiwa kuwasilisha ujumbe katika jamii za kisasa.

  • Tags

You can share this post!

VYAMA: Chama cha Kiswahili katika shule ya upili ya...

KAULI YA WALLAH: Ukitaka ufanikiwe zaidi sharti uwe...

T L