• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 1:47 PM
Hospitali 260 zafungwa kwa kutokidhi viwango

Hospitali 260 zafungwa kwa kutokidhi viwango

NA MWANDISHI WETU

BARAZA la Matabibu na Madaktari wa Meno (KMPDC) limefunga vituo vya huduma za afya visivyozingatia sheria na kanuni zilizowekwa.

Afisa Mkuu Mtendaji wa KMPDC Dkt David Kariuki akihutubia wanahabari jijini Nakuru mnamo Alhamisi amesema hospitali 260 kati ya 1,305 zilizokaguliwa kufikia Agosti 9, 2023, zimefungwa.

“Tulifanya ukaguzi wa vituo vya afya jijini Nairobi, Mombasa, Nakuru, Meru na Embu na vile ambavyo havijafuata sheria na kanuni vimefungwa,” amesema Dkt Kariuki.

Aidha, katika Kaunti ya Nakuru, jumla ya vituo 44 vimefungwa.

  • Tags

You can share this post!

Ruto: Kanini Kega alitusumbua chini ya utawala wa Jubilee...

Uchunguzi wazi wa kifo cha Jeff Mwathi waanza

T L