• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:33 AM
Jeneza la kilo 65, sawa na uzito wa Kiptum alipokuwa hai

Jeneza la kilo 65, sawa na uzito wa Kiptum alipokuwa hai

LABAAN SHABAAN, SAMMY WAWERU NA FRIDAH OKACHI

NYOTA wa marathon Kelvin Kiptum alipumzishwa akilazwa ndani ya jeneza la kahawia.

Jeneza lenye uzani wa kilo 65 lilibebwa na gari la kifahari kutoka mochari ya Eldoret kuelekea makao yake ya mwisho kijijini Naiberi, kaunti ya Uasin Gishu.

Si sadfa kuwa jeneza hilo lina uzito wa kilo 65. Hata uzani wa Kiptum mwenyewe unawiana na huu wa jeneza.

Msafara wa buriani kwa bingwa huyu ulitoa fursa kwa halaiki ya watu kumuaga.

Ni bayana rangi hii ilikusudiwa kuashiria Kiptum kuwa mtu mwenye uaminifu na uwazi.

Rangi hii ya mchanga inaonyesha mwanariadha mchanga aliyekuwa na nguvu na ustahimilivu.

Sifa hizi zilikuwa muhimu katika mbio za masafa marefu zinazohitaji mtu asiyechoka hadi apate anachotaka.

Ndivyo hivyo marehemu Kiptum alivunja rekodi ya dunia ya marathon na kuwa mwanariadha wa kwanza duniani kukimbia chini ya saa mbili na dakika moja.

Mnamo Oktoba 2023, Kiptum alistahimili mititigo huko Chicago nchini America na kuibuka mshindi kwa kutimka kwa saa 2 na sekunda 35.

Kijana wa umri wa miaka 24, alivunja rekodi ya mkimbiaji mashuhuri Eliud Kipchoge, 39, ambaye amesherehekewa duniani kwa miaka.

Katika uhai wake, Kiptum alishiriki marathon tatu na kushinda zote.

Akinakili kasi ya juu ya mbio hizi, orodha ya rekodi bora saba katika historia ya marathon duniani zimesheni ushindi wake.

“Ufanisi wa Kelvin si wa kawaida. Kwamba alifika viwango hivi katika umri mdogo, ni tukio la kipekee,” alistaajabu Rais wa Riadha Duniani Sebastian Coe.

Nyota huyo aliyekuwa baba wa watoto wawili, alifariki mnamo Februari 11, 2024, katika ajali ya barabara ya Kaptagat – Eldoret akiwa pamoja na kocha wake, Gervais Hakizimana (Mrwanda)

Siku chache kabla ya kifo chake, rekodi ya mwanariadha huyo ya saa 2 na sekunde 35 iliidhinishwa na Shirikisho la Kimataifa la Riadha Duniani.

  • Tags

You can share this post!

Mwanajeshi Mwingereza ajitetea akisema alipigwa Kiswahili...

MAONI: Afrika itapiga hatua hata zaidi watu wa nje wakiacha...

T L