• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 11:55 AM
Kiir apiga marufuku uimbaji wimbo wa taifa wakati hayuko

Kiir apiga marufuku uimbaji wimbo wa taifa wakati hayuko

MASHIRIKA Na PETER MBURU

RAIS wa Sudan Kusini Salva Kiir amepiga raia wa nchi hiyo kuimba wimbo wa taifa wakati wowote asipokuwa mahali panapoimbiwa.

Akitoa tangazo hilo, Waziri wa Mawasiliano nchini humo Michael Makuei Jumatatu alisema kuwa viongozi na mashirika mbali mbali yamekuwa yakiimba wimbo huo kwa kuuharibu, akisema hayo ni matumizi mabaya ya wimbo wenyewe.

“Kila mtu afahamu kuwa wimbo wa taifa ni wa Rais pekee, kwa hafla ambayo imehudhuriwa na Rais, si wa kila mtu,” akasema waziri huyo.

Alipuuzilia hali ya viongozi wengine kama mawaziri na magavana kuimbiwa wimbo huo wanapohudhuria hafla, akisema amri hiyo ya Rais Kiir ilipitishwa na baraza la mawaziri Ijumaa.

Alisema mahali pekee ambapo wimbo wa taifa unafaa kuimbwa ni katika balozi za taifa hilo ambazo zinawakilisha Rais, na mashuleni ambapo watoto wanafunzwa kuuimba. Kando na hayo, hakuna mtu mwingine anaruhusiwa kuuimba.

Aidha, waziri huyo alisema viongozi wa kijeshi hawaruhusiwi kuhutubia umma wanapokuwa wamevalia sare za kijeshi.

Hata hivyo, hakueleza adhabu ambayo watakaovunja sheria hizo watapokea, akisisitiza tu kuwa watakaozikiuka watakabiliwa.

You can share this post!

Mwanamume ashtaki korti kwa kumfanyia upasuaji wa...

Mwanamke amuua mwanamume aliyemzaba kofi

adminleo