• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 6:21 PM
KRU imani tele mashabiki wa raga watarejea viwanjani Desemba

KRU imani tele mashabiki wa raga watarejea viwanjani Desemba

Na GEOFFREY ANENE

SHIRIKISHO la Raga Kenya (KRU) limejaa matumaini kuwa mashabiki watarejea viwanjani kufikia mwisho wa 2021 baada ya marufuku ya karibu miaka miwili iliyosababishwa na mkurupuko wa janga la virusi vya corona.

Matumaini hayo, Mwenyekiti wa KRU Oduor Gangla anasema, yanatokana na tangazo la Rais Uhuru Kenyatta kuwa Kenya inalenga kuwapa watu 10 milioni chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi hivyo kufikia Desemba 2021 na watu 26 milioni ifikapo Desemba 2022.

“Imekuwa vigumu sana KRU kuvutia wadhamini bila ya mashabiki kuja viwanjani. Tunatumai kuwa kufikia Desemba mwaka huu mashabiki wataruhusiwa kuhudhuria mechi kwa sababu ya kuchanjwa ili pia shirikisho liweze kuimarisha hali yake ya kifedha kusaidia miradi mbalimbali tunayo,” aliambia Taifa Leo katika mahojiano ya kipekee.

Kabla ya kisa cha kwanza cha virusi vya corona kuthibitishwa nchini Kenya mnamo Machi 12 mwaka 2020, mashabiki walikuwa wanafurika katika viwanja vya mchezo wa raga kwa mechi za ligi pia za timu za taifa.

Kenya imeshuhudia visa 186,053 vya maambukizi ya corona na vifo 3,690 vinavyotokana na ugonjwa wa Covid-19. Watu zaidi ya 450,000 nchini Kenya wamepokea chanjo ya kukabiliana na virusi hivyo. Idadi ya watu Kenya ni karibu 52 milioni.

  • Tags

You can share this post!

Senegal yashinda Kundi B ya raga ya wachezaji 15 kila upande

Jumwa akwamilia UDA, adai Ruto ataingia Ikulu 2022