• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 12:48 PM
Masaibu: Bloga wa Azimio Pauline Njoroge akamatwa kwa madai ya ulanguzi wa mihadarati   

Masaibu: Bloga wa Azimio Pauline Njoroge akamatwa kwa madai ya ulanguzi wa mihadarati  

NA MWANGI MUIRURI  

IDARA ya polisi nchini imethibitisha kukamatwa kwa Naibu mratibu wa chama cha Jubilee, Bi Pauline Njoki Njoroge kwa madai ya kuwa mlanguzi wa mihadarati.

Aidha, anakabiliwa na madai mengine ya kutumia mitandao ya kijamii kueneza chuki katika jamii.

Kupitia taarifa rasmi ya kitabu cha matukio katika kituo cha polisi cha Watamu kilichoko Kaunti ya Kilifi, Bi Njoroge ambaye pia ni mwanablogu wa masuala ya Azimio la Umoja-One Kenya Coalition alikamatwa Julai 22, 2023.

Taarifa hiyo ilisema kwamba Bi Njoroge alikuwa katika gari moja akiandamana na Bi Jane Mwangi Nduta na Bw Emanze Jilani.

“Kwa pamoja walikuwa na bidhaa 64 ambazo zinashukiwa kuwa na makali ya mihadarati. Aidha, simu ya Bi Njoroge ilithibitishwa kutumika kueneza jumbe zinazokadiriwa kuwa hatari kwa uwiano wa umma,” taarifa hiyo inasema.

Iliongeza kuwa Bi Njoroge atashtakiwa mahakamani kutokana na kisa hicho.

 

[email protected]

 

 

  • Tags

You can share this post!

Omingo Magara alia ‘kucharazwa’ na baridi, amsihi Rais...

Viongozi, maafisa wa kiusalama Mlima Kenya walia...

T L