• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 12:15 PM
Mchezaji bora wa Julai Zambia ni Jesse Were, atuzwa Sh15,000!

Mchezaji bora wa Julai Zambia ni Jesse Were, atuzwa Sh15,000!

NA CECIL 0DONGO

MSHAMBULIZI wa timu ya Taifa Harambee Stars Jesse Were alitwaa tuzo ya mchezaji bora anayeenziwa sana na mashabiki mwezi Julai 2018 nchini Zambia baada ya kung’aa akiwajibikia Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini humo Zesco United.

Mwanadimba huyo alipigiwa kura na mashabiki wengi na kuibuka kidedea mbele ya mpinzani wake wa karibu anayesakatia Green Eagles, Anos Tembo baada ya raundi ya pili ya upigaji kura.

Katika raundi ya pili ya upigaji kura, Mkenya huyo alijizolea kura 1056 kati ya kura zote 1553.  Tembo alimfuata kwa karibu kwa kupata kura 498.

Hata hivyo mambo yalionekana kumwendea tenge Were katika raundi ya kwanza alipobwagwa na mpinzani wake kwa kura 406 dhidi ya 155 alizopata Were.

Were aliteuliwa kuwania tuzo hiyo kwa mara ya kwanza mwezi Juni lakini akaibuka katika nafasi ya tatu nyuma ya fowadi wa Power  Dynamos Alex Ngonga na mshindi  Spencer Sautu ambaye pia husakatia Green Eagles.

Mshambulizi huyo wa zamani wa Tusker sasa atapokea tuzo yake siku ya Jumapili wakati timu yake itakapochuana Napsa Stars ugeni.

Tuzo hiyo huandamana na kitita cha Sh15,000 ambacho hupokezwa mshindi. Ingawa hela hizo huenda zikaonekana kama kidogo mno machoni mwa Wakenya, nchini Zambia hizo ni hela nyingi tu za kustahili tuzo hiyo.

You can share this post!

Timu ya handiboli yaelekea Rwanda kusaka ubingwa wa Afrika

MABADILIKO SERIKALINI: Rais atuliza joto la kutimua baadhi...

adminleo