• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 9:50 AM
Merkel ang’atuka baada ya kuongoza Ujerumani miaka 16

Merkel ang’atuka baada ya kuongoza Ujerumani miaka 16

Na AFP

WAZIRI Mkuu wa Ujerumani, Angela Merkel ameng’atuka afisini baada ya kuongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 16.

Kiongozi mpya wa ujerumani sasa atakuwa Olaf Scholz, ambaye jana aliidhinishwa na bunge la nchi hiyo baada ya kufanikiwa kuunda muungano wa vyama vitatu ulio na idadi kubwa ya wabungeMerkel amekuwa kwenye siasa kwa miaka 31.

Scholz, 63, ambaye chama chake cha Social Democrats kilishinda viti vingi katika uchaguzi uliofanyika Septemba mwaka huu, alijipatia umaarufu alipokuwa naibu waziri mkuu katika serikali ya Merkel.Chama cha Social Democrats, hata hivyo, kilishindwa kupata idadi inayohitajika ya wabunge ili kuunda serikali.

Hii ilibidi Scholz kuunda muungano na vyama vya Greens na Free Democrats.Kiongozi wa chama cha Greens, Annalena Baerbock ameteuliwa kuwa waziri wa masuala ya kigeni katika serikali hiyo ya muungano. itakuwa na kibarua kigumu cha kupambana na maradhi ya corona huku taifa hilo likitarajia kushuhudia visa vingi vya maambukizi msimu huu wa baridi.

You can share this post!

Kocha wa AFC haendi popote- Shikanda

Museveni atetea kutuma jeshi DRC

T L