• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Mke aagizwa ashirikishe wapenzi wa kando wa mumewe katika usimamizi wa mali

Mke aagizwa ashirikishe wapenzi wa kando wa mumewe katika usimamizi wa mali

BRIAN OCHARO NA LABAAN SHABAAN

MJANE atawagawia wapenzi wa kando, mali ya thamani ya Sh54 milioni iliyoachwa na mume.

Wanawake hao wawili hawakuwa wameolewa kisheria kabla ya mume kufariki.  

Mali hiyo inajumuisha majumba katika kaunti za Mombasa na Taita Taveta.

Mahakama ya Masuala ya Familia Mombasa iligundua kuwa wawili hao hawakuwa wameolewa kisheria na hawakufaa kurithi mali hiyo.

Jaji Gregory Mutai aliamua wawili hao watasimamia mali kwa niaba ya watoto waliozaa na marehemu.

Kwa mujibu wa katiba, Jaji alitaja umuhimu wa urithi kwa manufaa ya watoto.

Alisema wanawake hao wanafaa kulinda maslahi ya watoto wao.

Jaji Mutai alitoa amri ya mali kusimamiwa na CWM (mke halali) na wake mipango ya kando – AA na KM.

Korti ilitupilia mbali ombi la KM kutaka kugawiwa mali KM aliposema alikuwa mke halali wa marehemu.

KM alienda kortini kupinga kutolewa kwa nyaraka za usimamizi wa mali.

Alisema alifaa kurithi mali ya marehemu sababu ya kuwa mke na mama wa watoto wa mwendazake.

KM alishikilia kuwa alitengwa makusudi kutoka kwa stakabadhi za usimamizi wa mali licha ya kuwa mnufaika halali wa mali.

Kulingana na KM, yeye alikuwa mke wa pili kupitia ndoa ya kitamaduni.

“Walalamishi wamepotosha korti kwa kuhusisha mtoto ambaye si mtoto halisi ama aliyechukuliwa na marehemu,” alisema.

KM alidai mtoto huyo alichukuliwa na mjane muda mrefu baada ya mume kufariki.

Ndoa ya miaka 15

Isitoshe, aliashiria mali yake binafsi iliwekwa visivyo pamoja na mali ya marehemu.

Hata hivyo, mjane (CWM) alipinga kuhusishwa kwa KM katika mali hiyo akisema ni yeye pekee alikuwa mke halali.

Alitoa cheti cha ndoa kilichoonyesha walifunga ndoa zaidi ya miaka 15 iliyopita.

Lakini aliridhia hatua ya watoto wa KM kufanywa wanufaika sababu walilelewa na marehemu nje ya ndoa.

Kuhusu mtoto anayedaiwa kuwa si mrithi halali, CWM alisema mtoto huyo alichukuliwa na marehemu kabla ya kufariki.

Vile vile alipinga madai ya mali ya KM kuhusishwa miongoni mwa mali inayorithiwa.

Kwa upande wake, AA alimpinga KM akisema alikuwa mjanja na asiyeshirikiana nao.

Alidai kuwa KM alipendelea mali ya marehemu ifaidi pia familia yake.

AA alijipigia debe kuwa mrithi halali kwa vile ana mtoto na mwendazake.

Katika uamuzi wa Jaji Mutai, CWM alitajwa kuwa mke halali na kwamba ndoa hiyo haikuwa ya mitara.

  • Tags

You can share this post!

Nazizi afunguka jinsi mwanawe mdogo alifariki wakiwa...

NASAHA ZA RAMADHANI: Tukague nafsi zetu msimu huu wa mfungo...

T L