• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 10:55 AM
Mzee, 80, atupwa jela miaka 20 kwa kumnajisi mjukuu

Mzee, 80, atupwa jela miaka 20 kwa kumnajisi mjukuu

NA RICHARD MUNGUTI

MZEE mwenye umri wa miaka 80 amehukumiwa kifungo cha miaka  20 jela kwa kumnajisi mjukuu wake kwa kipindi cha miaka mitatu kati ya 2017-2020.

Huku Samuel Githinji akitazamiwa kutoka jela akiwa na umri wa karne moja, hakimu mkazi wa Kandara Eva Wambugu alimfunga miaka 40 jela barobaro wa umri wa miaka 37 aliyempata na hatia ya kumdhulumu kimapenzi mpwa wake.

Katika kisa cha Githinji, hakimu alisema upande wa mashtaka ulithibitisha kabisa mshtakiwa alimdhulumu kimapenzi mjukuu wake.

Lakini hakimu alikataa ushahidi wa Githinji aliyedai aliwekelewa kutenda uhalifu huo na mkwewe aliyetalikiana na mwanawe.

Mahakama pia ilikataa ushahidi wa nyanya yake mlalamishi aliyeeleza korti akimtetea mumewe kwamba “hakushuhudia udhalimu ukifanyiwa mjukuu huyo wao.”

Lakini Bi Wambugu alisema mlalamishi alieleza jinsi babuye alikuwa anamtembelea usiku na kumdhulumu na wakati mwingine kujamiana naye wakiwa shambani.

“Hii mahakama imekubali ushahidi wa mlalamishi dhidi ya Githinji. Ni kweli alimnajisi. Hata ushahidi wa  daktari umethibitisha amenajisiwa mara kadhaa,” alisema Wambugu

Naye Gilbert Wanyoike alifungwa kwa kumchafua mpwawe.

  • Tags

You can share this post!

Daktari feki Mugo Wa Wairimu aongezewa adhabu ya jela miaka...

Makatibu: Kibarua kigumu kwa Ruto

T L