• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Okwiri aanza vyema kampeni ya kuwakilisha Kenya katika masumbwi Olimpiki 2020

Okwiri aanza vyema kampeni ya kuwakilisha Kenya katika masumbwi Olimpiki 2020

Na GEOFFREY ANENE

BONDIA Mkenya Rayton Okwiri alipiga hatua moja mbele kwenye kampeni ya kufika Olimpiki 2020 baada ya kushinda pigano lake la kwanza katika mashindano ya kuchagua wawakilishi wa Bara Afrika yanayoendelea jijini Dakar, Senegal.

Okwiri, ambaye jina lake la utani ni Boom Boom, alimshinda Emhemed Salem Elmagasbi kutoka Libya kwa wingi wa alama katika uzani wa kati (kilo 75) mnamo Alhamisi usiku.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 33 alisukumia Elmagasbi makonde mazito. Alikuwa na shabaha na kuibuka mshindi wa pigano hilo la kwanza japo alitatizwa kidogo na Elmagasbi katika raundi ya kwanza aliyepata Okwiri na makonde mazuri ya kushoto kisha kulia. Hata hivyo, kufikia katikati ya raundi ya pili, mambo yalikuwa magumu kwa Elmagasbi, ambaye alifurahi kuokolewa na mlio wa kengele ya kukamilisha pigano.

“Niliweza kutawala raundi zote tatu na kushinda mpinzani wangu kwa wingi wa alama. Hata hivyo, hicho kilikuwa tu kionjo,” alisema Okwiri.

Okwiri sasa atakabiliana na bondia anayeorodheshwa nambari moja katika ndondi hizi zisizo za malipo katika uzani huo barani Afrika, Kavuma David Ssemujju kutoka Uganda mnamo Februari 23.

Kikosi cha Kenya ambacho kiko Dakar:

Wanaume

Nick Okoth (Featherweight)

Rayton Okwiri (Middleweight)

Hassan Shaffi Bakari (Flyweight)

Elly Ajowi (Heavyweight)

Joseph Shigali (Lightweight)

Boniface Mugunde (Welterweight)

Humphrey Ochieng’ (Light Heavyweight)

Fredrick Ramogi (Super Heavyweight)

Wanawake

Elizabeth Andiego (Middleweight)

Christine Ongare (Flyweight)

Evelyne Akinyi (Lightweight)

Elizabeth Akinyi (Welterweight)

Beatrice Akoth (Featherweight)

You can share this post!

Brigid Kosgei amaliza katika nafasi ya pili Ras Al Khaimah...

Funzo kwa Uhuru

adminleo