• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 11:14 AM
Rangers kukutana na Malmo au HJK Helsinki katika mchujo wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA)

Rangers kukutana na Malmo au HJK Helsinki katika mchujo wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA)

Na MASHIRIKA

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

MABINGWA wa Ligi Kuu ya Scotland, Rangers, watakutana na Malmo au HJK Helsinki katika raundi ya tatu ya kufuzu kwa soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) muhua ujao.

Celtic pia kutoka Scotland wataonana na PSV Eindhoven au Galatarasay iwapo watawakomoa Midtjylland katika raundi ya pili ya mchujo.Chini ya kocha Ange Postecoglou, Celtic watamenyana na Midtjylland ya Denmark katika mchuano wa mkondo wa kwanza jijini Glasgow kabla ya kusafiri jijini Copenhagen kwa marudiano ya Julai 28.

Malmo kutoka Uswidi au HJK ya Finland itaalika Rangers ya kocha Steven Gerrard mnamo Agosti 3 au 4 kabla ya gozi la mkondo wa pili kupigiwa jijini Ibrox mnamo Agosti 10.Tarehe zizo hizo ndizo zitashuhudia Celtic wakinogesha mojawapo ya mechi za raundi ya tatu dhidi ya PSV ya Uholanzi au Galatasaray kutoka Uturuki.

Vikosi vitakavyoshinda mechi za raundi ya tatu zitafuzu kwa mchujo wa mwisho ambao utaandaliwa kwa mikondo miwili kati ya Agosti 17-18 na Agosti 24-25. Droo kwa ajili ya mchujo huo wa mwisho utafanyika Agosti 2.

Klabu zitakazopoteza michuano yao ya raundi ya tatu zitateremshwa kushiriki mchujo wa kufuzu kwa soka ya Europa League kati ya Agosti 19 na 26.Rangers wanajivunia kutinga hatua ya 16-bora ya Europa League katika kipindi cha misimu miwili iliyopita huku Celtic wakibanduliwa kwenye hatua ya makundi mnamo 2020-21 baada ya kuondolewa kwenye hatua ya 32-bora muhula uliotangulia.

Tangu kocha wa sasa wa Leicester City, Brendan Rodgers, aagane na Celtic mnamo 2017-18, taifa la Scotland halijawahi kuwa na mwakilishi katika soka ya UEFA. Rangers ambao ni washindani wakuu wa Celtic, walidenguliwa mapema katika hatua ya makundi ya UEFA mnamo 2010-11 chini ya kocha Walter Smith.

Mnamo 2011-12, Malmo waliokuwa wakitiwa makali na mkufunzi Ally McCoist, waliwabandua Rangers kwenye hatua ya makundi. Rangers ambao wamekuwa wakijivunia huduma za fowadi matata Alfredo Morelos tangu 2017, hawajawahi kukutana na HJK Helsinki ya Finland katika historia.

 

  • Tags

You can share this post!

Rashford kukaa nje kwa miezi miwili akiamua kufanyiwa...

Mbunge aomba msaada wa Rais kusaidia wahasiriwa wa mkasa wa...