• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Shamba la kuvuna upepo Marsabit

Shamba la kuvuna upepo Marsabit

NA RICHARD MAOSI.

JAMII za wafugaji wa maeneo kame ya Gatab na Mlima wa Kulal, Kaunti ya Marsabit wana mengi ya kujivunia mojawapo ikiwa ni shamba la kuvuna upepo.

Eneo hili linapakana na Kulal, msitu wa kipekee Afrika Mashariki unaozungukwa na jangwa la Chalbi upande wa Kaskazini na Ziwa Turkana sehemu ya Magharibi.

Shadrack Longoiyap mkazi wa Kulal ni mmoja wa afisa wa Mazingira, na anasema Marsabit vilevile inajivunia upepo mkali unaovuma kutoka nyanda za juu ambao huvunwa na hatimaye unatumika kuzalisha kawi ya umeme.

Anaungama kuwa sehemu kubwa ya Marsabit na Kaskazini Mashariki ya Kenya ni jangwa ila kuna mambo mengi ya kujivunia ambayo hayawezi kupatikana katika sehemu nyingine ulimwenguni.

Sehemu ya shamba la Msitu wa Kulal, linalotumika kuvuna upepo wa kawi Marsabit. PICHGA|RICHARD MAOSI

Anasema hili ni mojwapo ya shamba la kuvuna upepo na mara nyingi upepo huwa ni mkali majira ya asubuhi na kila ifikapo mwezi Oktoba.

“Makali yake hupungua alasiri na miezi ya Februari kila mwaka,” afisa huyo akaambia Taifa Leo Dijitali wakati wa mahojiano.

Mradi huu ambao umepatiwa jina la Lake Turkana Wind Power Project, unamilikiwa na wafugaji ikizingatiwa kuwa unaendeshwa katika ardhi ya jamii za hapa, ambazo zinamilikiwa na Samburu, Rendile, Elmolo na Turkana.

Nyimbo za kitamaduni ni kivutio cha Utalii kwa jamii nyingi za wafugaji hasa Wasamburu. PICHA|RICHARD MAOSI.

Aidha Taifa Leo Dijitali ilibaini, ukisimama juu ya vilima vya Mount Kulal Forest majira ya jioni kabla ya jua kuzama utafurahia kuvuta taswira nzuri ya Ziwa Turkana, ambapo unaweza kuhisi uko dunia yako.

Hii ikimaanisha kuwa wanaopenda kukwea milima wanaweza kufurahia mazingira ya hapa ikizingatiwa imegubikwa na milima na mabonde ambapo unaweza kuhisi uko dunia yako.

Hii ndio maana Umoja wa mataifa Chini ya mwavuli wa UNESCO, walitenga sehemu hii kuwa turadhi ya jamii na kivutio cha utalii.

Aidha nyimbo za kitamaduni ni kivutio cha Utalii kwa jamii nyingi za wafugaji hasa wasamburu.PICHA/RICHARD MAOSI.
  • Tags

You can share this post!

Karen Nyamu: Nilisaidia mke wa Samidoh kupata tenda 

GYM za mitaani Nakuru zatajwa kama majukwaa kufunza...

T L