• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 12:46 PM
‘Slay queens’ wadaiwa kuwinda mbegu za ‘mubaba’ kwa makahaba

‘Slay queens’ wadaiwa kuwinda mbegu za ‘mubaba’ kwa makahaba

NA MWANGI MUIRURI

BAADHI ya makahaba nchini inadaiwa huiba mbegu za wanaume na kuzibeba ndani ya mipira ya kondomu ambapo huziuza kwa matapeli wa kutaka wapate mimba kisha baadaye wasake malezi ya watoto na urithi wa mali.

“Ukizubaa na mbegu zako ovyoovyo ndani ya kondomu popote pale, wewe mwanamume umeshiriki ngono kiharamu, hasa ukiwa wewe ni tajiri, huenda ujipate mahakamani ukihukumiwa kulea mtoto au watoto na pia uwape urithi ukijua vizuri hujawahi kushiriki ngono na mama yao mzazi,” akasema mdokezi wetu.

Wakili David Kamau kutoka Kaunti ya Murang’a ameambia Taifa Leo kwamba “niko na kesi tatu kwa sasa ambapo kuna wanaume watatu waliofikishwa katika mahakama wakilazimishwa kulea watoto na watambue mama zao licha ya kuapa kwamba hawajawahi kuwa na uhusiano wa kimahaba na wanawake hao.

“Kwa sasa, uchambuzi wa DNA umefanywa na imebainika waziwazi kwamba baba wazazi ni hao wanaume na kwa sasa tunasaka kukata rufaa kwa msingi kwamba watoto hao walipatikana kupitia ujambazi ambao tunasaka ushahidi na sio suala rahisi,” akasema.

Wakili Kamau alisema mkondo wanaouchunguza ni kwamba huenda wanawake hao walitungwa mimba na jamaa wa washukiwa.

“Ingawa hivyo, kuna maafisa wa uchunguzi ambao tumesajili na ambao wamedokeza kwamba huenda mbegu za hawa wanaume ziliibiwa kupitia kashfa ya wizi wa mbegu ndani ya kondomu,” akasema wakili Kamau.

Mtaalamu wa Afya ya Uzazi Dkt Susan Mwikali ameambia Taifa Leo kwamba “mwanamke anaweza chini ya dakika 30 akachukua mbegu ndani ya kondomu na ikiwa yuko katika siku zile za uwezekano wa kushika mimba, akijimiminie mbegu hizo anaweza akashika mimba”.

“Mwanamume akishamwaga mbegu, zinaweza kuishi kwa kati ya dakika 15 hadi nusu saa. Lakini zikiwekwa katika barafu, zinaweza kaa milele hivyo basi kuwa rahisi kutekeleza wizi na zikatumike kutunga wengine mimba huko nje,” akaeleza Bi Mwikali.

Aliongeza kwamba mwachilio mmoja wa mbegu hizo huwa na idadi tosha ya kutunga mimba hata wanawake milioni moja hivyo basi mbegu za mwanamume mmoja zinaweza zikagawanywa huko nje ambapo kila mwanamke atajimiminia kidogo tu na nyingine kutumika kwa wengine.

Kulingana na wapelelezi, wanawake walio ndani ya ukora huu hufanya utafiti wa wanaume walio na mali na kutambua udhaifu wao wa kushiriki ngono kiholela.

“Huwa wanasaka makahaba ambao hushiriki ngono na wanaume hao na kuwalipa pesa ili wawaibie mbegu hizo zikiwa moto ndani ya kondomu. Mwanamume huyo anaweza kuwa yuko katika chumba kwa mfano ‘A’ huku naye mteja wa kujitunga mbegu akiwa amekodisha chumba nambari ‘B’ ili zikimwagwa tu atapewa kabla ya muda kuyoyoma na dili inaiva,” akasema mpelelezi huyo.

Kulingana na ufichuzi huo, ni sharti wanaume walinde mbegu zao kupitia kukataa kutolewa na makahaba mipira ya kondomu baada ya kushiriki tendo na pia kuhakikisha wameziharibu mara moja kabla ya kuibiwa.

  • Tags

You can share this post!

Murkomen afanya mabadiliko katika usimamizi wa KAA

Mwanamume afariki siku moja kabla ya kufunga pingu za maisha

T L