• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Stima kupotea usiku Jumatano, Alhamisi na Ijumaa

Stima kupotea usiku Jumatano, Alhamisi na Ijumaa

Na BERNARDINE MUTANU

Huenda maelfu ya wananchi wakasalia bila umeme kwa saa kadhaa baada ya kampuni ya Kenya Power kutoa ilani ya kufunga mfumo wa kununua umeme katika maeneo mengi humu nchini.

Kampuni hiyo imetangaza kuwa itafunga mfumo wake wa kununua stima (tokens) kwa lengo la kudumisha mfumo huo.

Mfumo huo utafungwa kuanzia saa nne usiku Jumatano (Novemba 7, 2018) kuanzia saa nne usiku mpaka Alhamisi saa kumi na mbili asubuhi (Novemba 8, 2018).

Mfumo huo utafungwa tena saa nne usiku Alhamisi mpaka saa kumi na mbili asubuhi Ijumaa (Novemba 9, 2018) kwa awamu ya pili.

“Wakati wa kipindi hicho, wateja wetu hawatakuwa na uwezo wa kununua umeme. Kenya Power hivyo inasahuri wateja wetu kununua umeme mapema kiasi ili kuepuka usumbufu katika kipindi hicho,” ilisema Kenya Power katika taarifa.

Kampuni hiyo ilisema hatua hiyo ni katika kuhakikisha utoaji mzuri wa huduma kwa wateja wake. Wiki jana, mfumo huo ulifungwa kwa lengo la kubadilisha aina ya malipo (tariff) kwa lengo la kuwafaa zaidi wananchi wa mapato ya chini.

You can share this post!

Ashtakiwa kumtenga mtoto na mama yake

Kansa imeua wanaume wengi kuliko wanawake – Utafiti

adminleo