• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:33 AM
Uchina mbioni kuunda mwezi bandia kupunguza gharama za stima

Uchina mbioni kuunda mwezi bandia kupunguza gharama za stima

BBC NA PETER MBURU

KAMPUNI moja ya Uchina imetangaza malengo yake ya kuweka ‘mwezi feki’ kwa ajili ya kuangaza zaidi wakati wa usiku.

Kulingana na gazeti moja la serikali ya taifa hilo, maafisa wa kampuni hiyo ya kibinafsi kutoka eneo la Chengdu wanataka kuzindua setilaiti hiyo ya kuangaza angani kufikia mwaka 2020, wakisema itaangaza vyema kiasi cha kuchukua nafasi ya stima za barabarani usiku.

Habari hizo sasa zimeibua uchangamfu, kejeli na maswali tele kutoka kwa watu mbalimbali, japo habari nyingi hazijatolewa kuhusiana na mradi huo.

Gazeti hilo wiki iliyopita lilimnukuu mwenyekiti wa kampuni hiyo ya Chengdu Wu Chunfeng akisema wazo hilo limekuwa likijaribiwa kwa miaka kadhaa na kuwa sasa teknolojia iko imara kutekeleza kazi hiyo, uzinduzi ukiwa wa 2020.

Gazeti la China Daily aidha lilimnukuu Bw Wu akisema kuwa “Vioo vikubwa” vinaweza kuzinduliwa 2022.

Hata hivyo, haikuwa wazi kutoka kwa magazeti yote ikiwa mradi huo unaungwa mkono na serikali ya taifa hilo.

Gazeti la China Daily liliripoti kuwa mwezi huo unaweza kufanya kazi kama kioo ambacho kitaakisi mwangaza wa jua usiku ili ufikie dunia.

Mwezi huo unatarajiwa kuwa kilomita 500 kutoka dunia, japo mwezi huwa kilomita 380,000 juu ya dunia.

Lakini ripoti hizo hazikueleza namna mwezi huo utakaa kwa umbo, lakini Bw Wu alisema utaakisi mwangaza kwa eneo la ukubwa wa kati ya kilomita 10 na 80 mraba, kwa mwangaza ‘mara sita’ ya ule wa mwezi.

Kampuni hiyo imesema kuwa mbinu hiyo inawezakuishia kuwa rahisi kigharama, ikilinganishwa na kulipia stima za barabarani.

Bw Wu alisema kuangaza eneo la Kilomita 50 mraba kunaweza kuokoa hadi dola 173 milioni za malipo ya stima kila mwaka.

Aidha, maafisa wa kampuni hiyo wamesema mwezi huo utaweza kuangaza maeneo yanayokumbwa na giza kama nyakati za mitetemeko ya ardhi.

“Stima ni bei ghali sana usiku, kwa hivyo tukiwa na mwangaza wa bure kwa miaka 15, itakuwa suluhu njema kiuchumi mwishowe,” mhadhiri wa chuo kikuu cha Glasgow Dkt Matteo Ceriotti akaeleza BBC.

You can share this post!

Ufadhili wa mabilioni kujenga nyumba za bei nafuu

Kigonya aishangaa Sofapaka kumnyima barua licha ya...

adminleo