• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 5:22 PM
Ujerumani, Italia na Uswidi watamba katika mechi zao za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2022

Ujerumani, Italia na Uswidi watamba katika mechi zao za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2022

Na MASHIRIKA

USHINDI wa 1-0 uliosajiliwa na Ujerumani dhidi ya Romania katika mechi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar sasa unawaweka kileleni mwa Kundi J kwa alama sita sawa na Armenia ambao pia walikomoa Iceland 2-0 katika mechi yao ya pili.

Goli la Ujerumani wanaotiwa makali na kocha Joachim Loew lilifumwa wavuni na kiungo mvamizi wa Bayern Munich, Serge Gnabry aliyeshirikiana vilivyo na kiungo wa Chelsea, Kai Havertz.

Ujerumani waliotawazwa mabingwa wa dunia mnao 2014 nchini Brazil, wangalifunga mabao zaidi katika gozi hilo lililochezewa jijini Bucharest ila fowadi Timo Werner akanyimwa nafasi za wazi na kipa Florin Nita.

Ujerumani watakuwa wenyeji wa Macedonia Kaskazini katika mchuano wao ujao mnamo Machi 31, 2021.

Italia wanaselelea kileleni mwa Kundi C kwa wingi wa mabao dhidi ya Uswisi baada ya kuwapiga Bulgaria 2-0. Ushindi huo wa Italia uliendeleza rekodi ya kutoshindwa katika jumla ya mechi 24 zilizopita chini ya kocha Roberto Mancini.

Nahodha Andrea Belotti aliyesaidiana na Federico Chiesa katika safu ya mbele alifungulia Italia ukurasa wa mabao kupitia penalti kabla ya mwisho wa kipindi cha kwanza baada ya kuchezewa visivyo na Daniel Dimov ndani ya kijisanduku. Manuel Locatelli alifungia Italia goli la pili katika dakika ya 82.

Uswisi waliwapepeta Lithuania 1-0, ila mchuano huo ukachelewa kuanza kwa dakika 15 kwa kuwa lango moja lilikuwa kubwa kuliko jingine uwanjani St Gallen Kybunpark. Bao la Uswisi lilifumwa wavuni na kiungo mvamizi wa Liverpool, Xherdan Shaqiri, katika dakika ya pili.

Katika mechi nyingine, Zlatan Ibrahimovic, 39, alichangia bao katika ushindi wa 3-0 uliosajiliwa na Uswidi dhidi ya Kosovo. Ludwig Augustinsson alifunga goli la kwanza la Uswidi kabla yam engine kufumwa wavuni kupitia Alexander Isak kiungo wa zamani wa Sunderland, Seb Larsson.

Kikosi hicho cha kocha Janne Andersson sasa kinaongoza Kundi B kwa alama sita, mbili zaidi kuliko Uhispania waliotawazwa mabingwa wa dunia mnamo 2010 nchini Afrika Kusini. Uhispania ya kocha Luis Enrique ilipepeta Gerogia 2-1 katika mechi nyingine ya Kundi B.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Aguero kuagana rasmi na Man-City mwishoni mwa msimu

Ibrahima Konate katika orodha ya wanasoka watano...