• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:53 PM
Upasuaji wa miili 10 ya wahanga Shakahola waonyesha walikufa njaa, ukosefu wa maji na watoto kunyongwa  

Upasuaji wa miili 10 ya wahanga Shakahola waonyesha walikufa njaa, ukosefu wa maji na watoto kunyongwa  

Na ALEX KALAMA

WATAALAMU wa upasuaji wamefanya upasuaji wa miili 10 ya wahanga wa imani potovu iliyofukuliwa Shakahola, Kaunti ya Kilifi.

Kati ya 10 hiyo, 9 ni ya watoto.

Upasuaji huo uliotekelezwa chini ya uongozi wa Mwanapatholojia Mkuu wa Serikali Dkt Johansen Oduor, umeonyesha waathiriwa walikufa njaa na kukosa maji.

Miili 2 ya watoto, uchunguzi uliashiria walifariki kwa sababu ya ukosefu wa hewa na kunyongwa.

Dkt Oduor alifichua kwamba watoto waliofanyiwa upasuaji , ni wa umri kati ya mwaka mmoja na nusu hadi kumi.

Mtaalamu huyo aidha alidokeza kuwa tayari miili hiyo ilikuwa imeanza kuoza.

“Familia ambazo zinatafuta wapendwa wao, Jumanne tutaanza kuchukua sampuli za DNA ili kuzilinganisha,” Dkt Oduor alisema.

Miili yote 10 ilikuwa na viungo vyote kamili.

Shughuli hiyo ilifanyika katika Mochari ya Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Malindi.

Mhubiri tata Paul Mackenzie wa Good News International Church, anahusishwa na maafa hayo.

Miili 110 tayari imefukuliwa shambani mwake, Shakahola.

  • Tags

You can share this post!

Mafuriko: Familia kadha Kisumu zaachwa bila makao, maafa...

Waziri Kuria: Tutapeleka maandamano kwa Kenyatta

T L