• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 5:22 PM
Ushirikiano Kaunti ya Kaimbu wainua wafugaji wa kuku

Ushirikiano Kaunti ya Kaimbu wainua wafugaji wa kuku

NA KEVIN ROTICH

Kabla ya ushirika wa wakulima wa kuku kuvumbuliwa mwaka jana katika eneo la Ngoingwa, wakulima wa kaunti ya Kiambu walikuwa wakizipitia changamoto tele kwenye mikono ya madalali.

Kile ambacho wakulima hawa walikuwa wakikosa ni uwezo wa uchumi, mikopo, masoko na pia vifaa vya ukulima kama vile malori na mashine .

“Mwezi wa Machi mwaka jana, kama wakulima wa kuku, tuliungana ili kukabiliana na changamoto tulizokuwa tukikumbana nazo kama vile ukosefu wa masoko, gharama ya juu ya vyakula vya wanyama na pia kuongezeka kwa mayai na nyama ya kuku kutoka mataifa jirani kama vile Uganda na Tanzania,” Mkurugenzi wa Ushirika wa kuku katika kaunti ya Kiambu Zack Munyambu anasema.

Wakulima wadogo wadogo kutoka kaunti za Eldoret, Muranga, Nairobi and Embu waliposikia mipango hii, pia wao waliomba wajumuishwe.

“Baadae, tulikubaliana wale ambao hawakuwa wanatoka kaunti yetu waunde zao kauntini mwao. Lakini, kuna wale ambao waliomba wajumuishwe kwenye kikundi chetu lakini bila uekezaji wowote,” anaeleza huku akiongezea kuwa walipokea cheti cha usajili mwaka jana.

Wakiwa na Sh760, 000 ya kuwekeza, walinunua shamba, mali ghafi ya kutengeza chakula ya wanyama na pia magari ya kusafirisha vyakula hivyo.

“Mwaka mmoja baadae, tunajivunia zaidi ya Sh4 milioni,” anasema.

Kutoka wanachama chini ya 250 walipoanza, wanachama wao sasa ni zaidi ya 700 members katika kaunti ndogo za Thika, Gatundu North, Gatundu South and Juja.

Kutokana na ushirikiano huo, walifungua kikundi cha WhatsApp ambacho kingewawezesha wakulima kupokea mawaidha kutoka kwa wataalam wa kuku na baadae kupata wosia kamili.

“Ikiwa kuku wa nyama, wa kutaga au kienyeji ya mkulima ikiwa mgonjwa, tunawaunganisha na agrovets and veterinarians,” ananena.

Christopher Kimani, ambaye ni mkulima wa kuku katika kaunti hii anasema kabla ya kikundi hicho kiundwe wakulima walikumbana na matatizo ya kupata soko na wosia wa wataalam.

Hapo mbeleni, nilipata hasara kubwa kwa mapato na mazao kwani sikuwa na mtu wa kumtegemea kwa wosia.

“Kupata wateja ilikuwa kazi ngumu kwa sababu kulikuwa na wakulima wengi wa kuku ya mayai na nyama ambao walingangania wateja wachache. Pia nyama ya bei nafuu kutoka mataifa jirani kama vile Tanzania na Uganda pia ilichangia. Wakati mwingine ilinibidi niuze kwa bei ya kutupa,” anasema.

Pia wana kiwanda cha kutengeneza vyakula vya wanyama ambazo uuzwa kwa wanachama kwa bei ya chini ambayo wanaweza kugaramia na pia kwa mkopo.

“Tunauza vyakula vya wanyama kutoka Sh300 hadi Sh400  ka guni la kilo 75 kwa wanachama wetu,” anaongezea.

Bwana Kimani anaongezea kuwa kupata pembejeo za shamba kama vile vya kulisha kuku ilikuwa vigumu apo mbeleni kwani hawangezipata bila mkopo.

“Na kiwanda hichi, ninaweza kupata chakula ya kuku wa mayai kwa mkopo alafu nilipe baadae nitakapo uza kuku wangu,” anasema.

Wanatengeza vyakula vya bata mzinga, nguruwe na bata wa kawaida. “Kwa ngombe wa maziwa, tunazo lishe a kawaida ambazo ni unga uliosagwa vyema na kuongezewa virutubishi vya madini muhimu,” anasema.

“Tunaitisha malighafi kutoka mataifa kama vile Tanzania, Uganda and Zambia. Lakini, tunapata maize kutoka bonde la ufa na pia maeneo ya mashariki,”

Kwa sasa, wameajiri watu kumi na saba ambao wanafanya kazi katika sekta kama vile administrative, transportation and animal feed factory.

Katika mwisho wa kila mwaka, wanachama watapokea faida kulingana na maekezo zao na pia mapato ya kampuni.

Ann Ngugi anasema kila mara wanaenda benchmarkings amabyo inawapa maelezo na tajriba ya kukuza kuku. “Hapo awali, hatungeweza kushirikiana pamoja,” Bwana Ngugi anasema.

You can share this post!

Soko la Uhuru linavyowapa riziki wafanyabiashara Nairobi

Watambue baadhi ya Waganda waliowahi kusakatia K’Ogalo