• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 5:22 PM
Wachuuzi 500 wakosa pa kuuzia baada ya vibanda kubomolewa Muthurwa

Wachuuzi 500 wakosa pa kuuzia baada ya vibanda kubomolewa Muthurwa

Na SAMMY KIMATU

MUTHURWA, NAIROBI

MAMIA ya wachuuzi wamekosa pahali pa kuuzia bidhaa baada ya vibanda vya kubomolewa kupisha ujenzi wa ukuta.

Aidha, hali hiyo ilitokana na hatua ya Idara ya Huduma za Jiji la Nairobi (NMS) kumpa mwanakandarasi mmoja kazi ya kujenga ukuta wa mawe unaozunguka Soko la Muthurwa huku vibanda vya wachuuzi hao vikibomolewa.

Awali, wachuuzi hao wapatao zaidi ya 500 waliuza bidhaa katika nafasi zilizokuwa wazi kwenye ua la kwanza uliokuwa na mashimo yaliyokuwa katikati ya vyuma.

Isitoshe, wauzaji waliuzia wateja wakiwa ndani ya vibanda upande wa ndani wa soko nao wanunuzi wakiwa upande wa nje ya soko.

Vibanda vyao vilikuwa takribani urefu wa mita 300 mkabala wa barabara ya Ladhies na pande wa kulia kwa barabara ya Haille Sellasie.

Mwenyekiti wa soko hilo, Bw Nelson Githaiga Waithaka aliambia Taifa Leo kwamba hili ni pigo kwa wafanyabiashara hao baada ya pigo lingine mbapo wachuuzi wengine zaidi ya 500 kufurusha sokoni hilo sawia na soko la Wakulima baada ya kampuni ya Reli kujenga ua mapema mwaka huu.

“Hili ni pigo la pili watu wakifurusha sokoni wakati huu kuna ukosefu wa ajira baada ya janga la Corona kuripotiwa nchini. Soko hili lilifunguliwa rasmi na aliyekuwa rais wa Kenya, Bw Mwai Kibaki kama njia moja ya wananchi kusukuma gurudumu la maisha kwa kujiajiri,” Bw Githinji akasema.

Bw Githaiga, alliiomba NMS kushawishi mwenye kandarasi ya kujenga ukuta kuwajengea wachuuzi hao vibanda vizuri punde atakapomaliza ujenzi ili wafayabiashara wazidi kuchapa kazi.

Vilevile, Bw Githaiga alishukuru NMS kwa kuipa soko la Muthurwa sura mpya kupitia maendeleo yanayaofanyika ndani ya soko hilo ikilinganishwa na awali soko ilipokuwa chini ya usimamizi wa serikali ya Kaunti ya Nairobi.

Mwenyekiti huyo aliiuliza NMS kuzindua kisima lilichochimbwa ndani ya soko la Muthurwa akiongeza kwamba mradi wa kisima ulikamilika mwaka jana.

Aliongeza kwamba huu ni wakati mwafaka wa wananchi kutumia maji kutoka kisima hicho wakati huu wa corona.

“Tunalazimika kununa maji ya kunawa mikono tukiwa sokoni tunapodumisha kuzuia msambao wa corona kwa mujibu wa wizara ya afya lakini changamoto kubwa ni kucheleweshwa kwa maji ya kisima kuzinduliwa rasmi ilhali mradi wa ujenzi wa kisima upo tayari baada ya kukamilika mwaka jana,’’ Bw Githaiga akaelezea.

  • Tags

You can share this post!

Wavamiwa na nyuki baada ya kuiba mtungi wa gesi na...

Wakenya wakerwa na mbunge kuzindua televisheni