13 wauawa polisi wakipambana na wahalifu Mexico

13 wauawa polisi wakipambana na wahalifu Mexico

NA AFP

GUADALAJARA, Mexico

WATU 13 waliuawa katika makabiliano ya risasi kati ya polisi na wanachama wa genge moja la wahalifu katika jimbo la Jalisco nchini Mexico, watawala walisema Alhamisi jioni.

Makabiliano yalitokea usiku katika kitongoji cha El Salto viungani mwa jiji la Guadalajara, mashahidi walisema.

Miili ya watu tisa, akiwemo mwanamke, ilipatikana ndani ya nyumba fulani katika mtaa huo, maafisa wa usalama walisema.

Maafisa wanne wa polisi pia walifariki katika patashika hiyo ya ufyatulianaji risasi.

“Watu wawili walioshikwa mateka ndani ya jengo waliokolewa baada ya habari kutolewa kwamba watu waliojihami kwa bunduki walionekana wakiwaingiza watu ndani ya nyumba hiyo,” Luis Mendez Ruiz akawaambia wanahabari.

  • Tags

You can share this post!

IEBC yaita wawaniaji Jumatano

Mwamerika Fred Kerley afuta muda bora wa mita 100 alioweka...

T L