Habari MsetoSiasa

2022: Jamii ya Abagusii yamtaka Matiang’i awanie urais

December 27th, 2018 1 min read

Na Eric Matara

MBUNGE wa Nakuru na baadhi ya viongozi kutoka Kaunti ya Kisii wamependekeza Waziri wa Usalama wa Ndani, Dkt Fred Matiang’i awanie urais 2022.

Mbunge wa Nakuru Town West, Bw Samuel Arama siku ya Krismasi aliongoza viongozi kutoka Kisii kumuunga mkono Dkt Matiang’i kwa wadhifa huo.

Hata hivyo, hatua hiyo inatarajiwa kuzua mjadala wa kisiasa. Walisema Matiang’i ndiye anafaa zaidi kumrithi Rais Uhuru Kenyatta.

“Ndugu yetu Matiang’i amefanya vyema katika majukumu yake kama waziri. Tunaamini kuwa ndiye mgombeaji bora zaidi wa urais 2022,” alisema Bw Arama.

Mbunge huyo alisema hayo alipoandalia wakazi wa eneobunge hilo Krismasi eneo la Londan.

“Dkt Matiang’i amethibitisha kuwa anaweza kwa kuzingatia wizara zote alizohudumu ikiwemo Elimu, Habari, Mawasiliano na Teknolojia. Ni mwenye bidii na hawezi kuvumilia utundu,” alisema mbunge huyo.