Kimataifa

Amerika yafuta hati ya kumwezesha Bensouda kuingia nchini humo

April 6th, 2019 1 min read

Na MASHIRIKA

THE HAGUE, Uholanzi

AMERIKA imemzima kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya uhalifu wa kimataifa (ICC) Fatou Bensouda, kuingia humo, afisi yake ilisema Ijumaa.

Hii ni kufuatia hatua ya Bensouda kuanzisha uchunguzi kuhusu uwezekano wa wanajeshi wa Amerika kutekeleza uhalifu wa kivita nchini Afghanistan.

Kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu (ICC) Fatou Bensouda. Picha/ AFP

“Tunaweza kuthibitisha kuwa serikali ya Amerika imefutilia mbali visa ya kumwezesha kiongozi wa mashtaka kuingia nchini humo,” afisi ya Bensouda iliviambia vyombo vya habari kupitia baruapepe.

Afisi hiyo ilisema kuwa hatua hiyo itamzuia kabisa Bensouda kusafiri nchini Amerika kutekeleza majukumu yake katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa (UN).

Japo mahakama hiyo ya ICC, yenye makao yake makuu jijini The Hague, Uholanzi sio mahamaka ya UN, Bensouda huenda Amerika kila mara kufahamisha Baraza la Usalama la UN kuhusu kesi zilizowasilishwa katika mahakama.