Habari Mseto

3 ndani miaka 90 kwa wizi na unajisi

February 6th, 2019 1 min read

Na Titus Ominde

MAHAKAMA moja mjini Eldoret imewafunga wanaume watatu miaka 90 jela kila mmoja, Baada ya kupatikana na hatia wizi wa mabavu na unajisi.

Watatu hao Isaac Maiyo Bett, Gilbert Manase Lime na Josphat Kipruto Bett walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kutumia nguvu kumwibia Bi Belinda Wamalwa kipakatalishi, simu mbili za mkononi aina ya Nokia na Samsung, mashine ya DVD, mashine ya michezo al maarufu home theatre, viatu jozi mbili, sketi tano, kuku wanane, vioo sita, bata mmoja miongoni mwa mali nyingine inayokisiwa kuwa ya kima cha Sh200,000 katika kijiji cha Bandari eneo la Mwamba kaunti ndogo ya Lugari,kaunti ya Kakamega mnamo Januari 3, 2016.

Bali na mashtaka hayo vile vile walipatikana na makosa matatu kila mmoja kwa kunajisi watoto watatu katika boma hilo wakati wa uvamizi husika.